Thursday, August 8, 2013
MWALIMU WA SHULE YA MSINGI APIGWA NA KUUAWA MKOANI DODOMA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA IMANI ZA KISHIRIKINA
Na John Banda, Dodoma
MWALIMU wa shule ya msingi Manchali Leah Goden 50 ameuawa kikatili na watu wanaodaiwa wenye hasira kali kutokana na kumtuhumu kujihusisha na ushirikina.
Mwalimu huyo alihusishwa na tukio hilo la ushirikina kutokana na vifo vya watu 4 wakiwemo watoto wake wawili, Mpenzi wake na Mwalimu mkuu wa shule anayofundisha kwa kipindi cha miaka miwili.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Alhamis hii majira ya saa 5 usiku ambapo kundi la watu wanaodaiwa wenye hasira kali walivamia nyumbani kwa mwalimu huyo na kumuua kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kichwani na ubongo kusambaa.
Mwili wa Mwalimu mkuu wa shule hiyo Florian Mligo umezikwa nyumbani kwao Songea ambapo inadaiwa alianza kuugua Tumbo na kugundulika utumbo wake ulikuwa umetoboka, hisia za wananchi ni kuwa aliwekewa sumu au uchaawi kwenye pombe na Mwalimu huyo walipokuwa wakinywa pamoja.
Mashuhuda wanasema sumu hiyo aliiweka kwa hasira kutokana na mkuu huyo wa shule kuanza kufuatilia mirath ya Marehemu Mwalimu mkuu msaidizi Adof Maunga aliyefariki feb 5 mwaka huu kwa madai kama hayo ya kuwekewa sumu kwenye pombe na mwalimu Lea walipokuwa na mahusiano ya kimapenzi.
“Angalia usije tutaja majina yetu gazetini, Inawezekana kulikuwa na faida aliyokuwa akiipata Lea kutokana na kuua mwaka juzi aliua wanae wawili mfululizo tena katuulia walimu wa watoto wetu lazima wananchi wapate hasira hizi’’
“Ona usiku wa kuamkia leo watu hawajalala wamekesha wakifurahia kwa kunywa pombe huku wakishangilia kama timu iliyopata ushindi kutoka na wengi walikuwa na hofu ya kunywa hasa wanapomkuta baa au kirabuni’’, alisema Baba wa makamo na kukataa kutajwa jina lake
Diwani wa viti maalum kata ya Chalinze Marry Mazengo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi wasijichukulie sheria mikononi badala yake waende kwenye vyombo vya sheri kama kuna mtu wanamuhisi kwa lolote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment