Saturday, August 31, 2013

KAMA KAWAIDA KIJANA KUTOKA MOROGORO FRANCIS CHEKA AMKALISHA PHIL WILLIAMS KUTOKA MAREKANI

  Bondia Mmarekani Phill Williams (kulia) akichapana na Francis Cheka wa Tanzania katika pambano lao lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
                                             hapa ngumi zimekolea kisawasawa .
Waziri wa Habari, Fenella Mukangara (wa pili kushoto) akimvisha Mknda wa Ubingwa wa Dunia wa WBF Bondia Francis Cheka baada ya kumchapa kwa Pointi mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, katika pambano lao la raundi 12 lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.

Friday, August 30, 2013

WASIFU WA MAREHEMU BABA ASKOFU MOSES KULOLA.



Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.
Ni mume wa Elizabeth na wamezaa watoto10 ambapo saba bado hai.alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.

Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.

Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.

Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuna makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo
Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila.
 

Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake. Nampenda sana Askofu Moses Kulola maana anafanya kazi ya MUNGU kwa moyo na kwa mujibu wa kitabu cha historia yake Askofu Kulola amezunguka Tanzania nzima tena wakati mwingine kwa kutembea kwa miguu na kwenye mazingira magumu sana kiasi kwamba ni wito mkuu wa MUNGU mkuu alionao Askofu Kulola na kwa miaka zaidi ya 60 amekuwa akihubiri neno la MUNGU na hadi sasa MUNGU anamtumia sana, katika mkutano uliopita wa askofu Kulola pale viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam maelfu ya watu walihudhulia na wengi sana kufunguliwa na injili anayohubiri askofu Kulola ni injili iliyonyooka na akiwataka wanadamu kumpa YESU KRISTO maisha yao ili wapate uzima wa milele bure.

Ukiacha mengi ambayo Mungu anaendelea kumtumia mtumishi wake huyu, kuna suala la nywele zake, askofu Kulola kama tulivyowahi kuandika siku zilizopita, hajanyoa nywele zake kwa takribani miaka 47 sasa, kwakuwa hakupendezwa na suala la kwenda salon kunyoa nywele zake hivyo akamwambia Mungu nywele alizokuwa nazo kwa wakati huo zisikue zaidi au kupungua, na ndivyo ilivyo mpaka sasa wembe haujapita kichwani mwake.

Thursday, August 29, 2013

BREAKING NEEEEEWZ!!!!! MAJAMBAZI YACHUKUA PESA KIULAIIINI AFRICAN BENKI KARIAKOO.

HABARI ZILIZOUFIKIA MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINASEMA KUWA WATU WANAODAIWA KUWA MAJAMBAZI WAMEINGIA KATIKA BENKI YA 'AFRICAN BANK' ILIYOPO MTAA WA LIVING STONE KARIAKOO HUKU WAKIWA WAMEVALIA MAVAZI YA JESHI LA POLISI, WAKIWA NA SILAHA NA GARI AINA YA NOAH NA KUCHUKUA PESA KILAINI NA KUONDOKA ZAO.

IMEELEZWA KUWA MAJAMBAZI HAO WALIPOFIKA NDANI YA BENKI HIYO WALIJITAMBULISHA KUWA WAMEFUATA PESA ZA KUPELEKA BENKI KUU AMBAPO WALIPEWA MZIGO WOTE HUKU NDANI YAKE KUKIWA NA PESA ZA KIGENI NA ZA TANZANIA NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA.

AIDHA IMEELEZWA KUWA BAADA YA WATU HAO KUTOKA NJE YA BENKI HIYO WALIINGIA KWENYE GARI HIYO NA KUONDOKA NA BAADA YA DAKIKA KADHAA WAHUSIKA WALITOKA NJE NA KUANZA KUPIGA KELEE ZA KUITIWA ''WEZI WEZI JAMANI MAJAMBAZI, WAMETUIBIA''.

LAKINI KELELE HIZO HAZIKUZA MATUNDA KWANI WATU WALIBAKI WAKIDUWAA KWA JINSI WATU HAO WALIVYOKUWA WAKIONEKANA KAMA ASKARI WANAOSINDIKIZA MAGARI YENYE PESA NA WAO PIA WAKIJUA NI KAMA KAWAIDA YA MAGARI YANAYOFIKA KATIKA BENKI HIYO KUCHUKUA PESA KWA AJILI YA KUPELEKA BENKI KUU. 

HABARI HIZI ZIMEDHIBITISHWA NA KAMANDA WA POLISI WA KANDA MAALUM, SULEIMAN KOVA, ALIYESEMA KUWA NI KWELI TUKIO HILO LIMETOKEA LEO ASUBUHI MAJIRA YA SAA TATU KASORO NA KWAMBA ATATOLEA UFAFANUZI KAMILI JUU YA TUKIO HILO BAADA YA KUPATA TAARIFA KAMILI LEO.

BREAK NEWS:ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA.

TAARIFA ZA HIVI PUNDE ZILIZOFIKA KWENYE CHUMBA CHA MTANDAO WETU NI KWAMBA MTUMISHI WA MUNGU ASKOFU MOSES KULOLA AFARIRIKI DUNIA

KUFUNGWA KUBAYA SANA CHUJI AMFUATA MWAMUZI CHUMBANI KUTAKA KUMDUNDA KATIKA MCHEZO KATI YA YANGA NA COASTAL UNION.

Askari Polisi wakimzuia Kiungo Mkabaji wa Yanga, ambaye ni majeruhi, Athuman Idd 'Chuji' aliyechukizwa na uchezeshaji mbovu wa mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Coastal, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, leo jioni. 

Chuji alikuwa akimsaka mwamuzi huyo ili kumtia adabu kutokana na maamuzi yake ya kuwapa penati wapinzani wao ambayo wao waliielezea kuwa haikuwa sahihi. Mwamuzi huyo Martin Saanya, alitoa penati katika dakika ya 90+ kwa kile kilichoonekana kuwa Beki wa Yanga David Luhende aliunawa mpira huo, huku mshika kibendera wake akiwa karibu kabisa na eneo la tukio na kushindwa kutoa maamuzi kwa kumsaidia mwamuzi wake ambaye alipuliza kipyenga cha kuashiria mkwaju wa penati hiyo iliyowakasilisha mashabiki na wachezaji wa Yanga.

Katika mchezo huo Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji wake, Didier Kavumbagu, katika dakika ya 68, kufuatia pasi nzuri iliyopigwa na David Luhende, na Coastal, walisawazisha bao hilo kwa mkwaju huo wa penati uliopigwa na Jerry Santo.

MACHINGA DODOMA WAKAIDI AGIZO LA MANISPAA.


 

Na John Banda, Dodoma

Wafanyabiashara ndago ndogo [Machinga] wamekaidi agizo la Manispaa ya Dodoma la kuwataka wasijenge vibanda katika stendi ya Daladala ya Jamatini mpaka watakapopewa utaratibu.
Machinga hao waliamua kuanza ujenzi mara tu baada ya kamati ya Mipango miji kuondoka katika eneo hilo walipofika kukagua na kufanya uhakiki wa waliokuwepo kabla ya ujenzi wa stendi hiyo kuanza Augost 2012  kama utaratibu ulifuatwa wakati wa ugawaji wa nafasi za kujenga  vibanda katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Machinga hao Haji Kulaya aliwatangazia wanachama wake kuwa waendelee kujenga vibanda vyao ili waweze kuanza biashara zao zilizosimama siku nne zilizopita tangu walipohamishwa toka ilipokuwa standi ya muda ya oil com.
Kulaya alisema wajenge kwa kutumia utaratibu wa walioutumia viongozi kugawa namba zenye majina ya machinga hao huku wakiuka agizo la Mwenyekiti wa kamati ya Mipango Miji Stephen Mwanga aliyewataka kutofanya chochote mpaka watakapopewa maelekezo toka manispaa.
Kamati hiyo ilifika katika stendi hiyo na kutokana na kupokea malalamiko toka miongoni mwa machinga hao ambao hawakuwa wamelidhika kutokana na kuwatuhumu viongozi wao kugawa nafasi kwa upendeleo huku wakiwaingiza watu ambao hawakuwepo awali katika stand hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na mazingira manispaa Stephen Mwanga  alikaliliwa kuwa walifika na kuamua kufanya uhakiki kwa wafanyabiashara hao na jumla yao ni 88 tofauti naya viongozi wao waliokuwa na 122 huku wageni hasa wanawake wakipewa kipaumbele.
“Tuliamua kufanya uhakiki ule kwa kutumia watu halisi waliokuwepo kwamaana walijuana kila mtu na jirani yake, tuligundua mama lishe 14, wenye vibanda 69, ugogo na upendo Group 7 jumla 88, huku waliokuwa na mezana,mboga mboga na matunda watafanyiwa utaratibu maarumu ili kuondoa malalamiko”, alisema Mwanga
Aidha aliongeza kuwa wao kama manispaa wenye stend na watu walifika ili kuondoa kelo na malalamiko yaliyokuwepo lakini kama watajenga bila mikataba wajiandae kuondolewa na wasimulaumu mtu nguvu ya Dola itakapotumika.
Kwa upande wake Naibu Meya manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede alisema kutokana na ujenzi wa stendi hiyo kugharim Mabilion ya Fedha wamepanga vibanda vyote vitakavyowekwa katika stend hiyo kuwa na paa moja, Rangi Moja na viwekwe kwenye mcholo.
Ngede aliongeza kuwa watahakikisha kila mtu atakaepata nafasi katika stendi hiyo wataingia nae mkataba na kutokana na orodha waliyo nayo itakuwa rahisi kujua machinga hao wataiingizia Halimashauri pato kiasi gani katika makusanyo.
“Tumejenga Stendi ya Kisasa na kutokana na kuwa huu ni mji wa makao makuu lazima kama inavyo ng’a hivi ndivyo iendelee Kung’aa hata na kwa wenye vibanda ili waendane nayo, na kutokana na mkataba hatutasumbuana na mtu juu ya ukusanyaji wa mapato”, alisema Ngede.   

Wednesday, August 28, 2013

BREAKING NEEEEEWZ!!!! BASI LA HOOD LAGONGA NA KUUA MMOJA PAPO HAPO.


HABARI ZILIZOUFIKIA MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINASEMA KUWA MTU MMOJA ANAYEKADILIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA (45) AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA BASI LA HUD LILILOKUWA LINATOKEA KILOMBERO KUJA JIJINI DAR, ENEO LA KIEMBENI MIKESE.

IMEELEZWA KUWA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE 15 WAMEJERUHIWA WAKATI BASI HILO LILIPOKUWA LIKIJARIBU KUMKWEPA MTU HUYO NA KUINGIA PORINI NA KISHA KUPINDUKA MIGUU JUU.

AIDHA IMEELEZWA KUWA DEREVA WA BASI HILO LILILOSABABISHA AJALI HIYO KUTOKANA NA MWENDO KASI, ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HASSAN MBEGA, AMETOROKA NA JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA ZOEZI LA KUMTAFUTA ILI KUMFIKISHA MBELE YA SHERIA.

MAJERUHI WAMEPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO KWA MATIBABU.

BREAKING NEEEEEEWZ!!! WATU 13 WAFA NA 11 MAJERUHI AJALI MBAYA MKOANI SHINYANGA.

HABARI ZILIZOUFIKIA MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINASEMA KUWA WATU 13, WAMEFARIKI DUNIA NA 11 WAMEJERUHIWA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA KIJIJI CHA NGONGWA MKOANI SHINYANGA KWENYE AJALI ILIYOHUSISHA GARI AINA YA HICE LENYE NAMBA ZA USAJIRI T 756 CHX NA GARI LILILOKUWA LIMEHARIBIKA LENYE NAMBA ZA USAJILI T 696 AMS.

AKIZUNGUMZA KWA NJIA YA SIMU KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA SHINYANGA, KIHEMA KIHEMA, ALISEMA KUWA MIONGONI MWA WATU WALIOFARIKI DUNIA NI PAMOJA NA DEREVA WA HICE, ILIYOKUWA NA ABIRIA HAO IKITOKEA KAHAMA KUELEKEA USHIROMBO AMBAYE ALIFARIKI PAPO HAPO, HUKU MAJERUHI WAKIPELEKWA KUPATIWA HUDUMA YA KWANA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.

KAMATI KUU YA CCM YATEGUA KITENDAWILI BUKOBA YABATILISHA MAAMUZI YA HALMASHAURI KUU YA MKOA ILIYOWAFUKUZA MADIWANI 8.



 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imejadili na kutolea maamuzi pamoja na mambo mengine suala la Madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera.


Katika maamuzi yake, Kamati Kuu imebatilisha uamuzi uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM ya Mkoa wa Kagera Agosti 13, 2013 wa kuwafukuza uanachama Madiwani hao. Hivyo Madiwani hao wanane ni wanachama halali wa CCM.
Kamati Kuu imetoa uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera haikuzingatia Katiba ya CCM ya 1977 Toleo la 2012 Ibara ya 93 (15). Ibara hiyo inasomeka kuwa moja ya kazi ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ni:-
“Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, isipokuwa kwa suala la kumvua uanachama au uongozi Diwani lisifanyike hadi Kamati Kuu imearifiwa na kutoa maelekezo”.
Aidha, Kamati Kuu imewaonya Madiwani wa CCM wa Manispaa ya Bukoba, Mbunge wa Bukoba Mjini na Meya kwa kusababisha kukosekana kwa utulivu, mshikamano na amani katika Manispaa na Chama.
Kamati Kuu pia imeitaka Serikali kumwagiza mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali(CAG) kufanya ukaguzi maalum wa haraka wa mambo yanayolalamikiwa dhidi ya Meya ili ukweli ujulikane na matokeo ya uchunguzi huo yasilishwe kwenye baraza la madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazoongoza Serikali za Mitaa.
Wakati tuhuma hizo dhidi ya Meya zikichunguzwa; Kamati Kuu inawataka Madiwani wa CCM  kurejesha utulivu kwenye Manispaa na Chama kwa ujumla ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi wa Bukoba.


Tuesday, August 27, 2013

MWENYEKITI WA MIPANGO MIJI NA MAZINGIRA MANISPAA YA DODOMA APIGA STOP UJENZI WA VIPANDA VYA BIASHARA STAND YA DALADALA JAMATINI.


Na John Banda, Dodoma
MWENYEKITI wa kamati ya Mipango miji na Mazingira Manisipaa ya Dodoma Stephen Mwanga Amesimamisha ujenzi wa vibanda vya wafanya Biashara ndogondogo [machinga] katika stend ya Daladala ya Jamatini baada ya kutolidhishwa na Ugawaji wa nafasi zao.
Machinga hao wamesimamishwa kujenga siku ya kwanza tangu stend hiyo kuanza kutumika baada ya kufungwa mwaka mmoja uliopita ili kupisha ujenzi utakaokidhi haja ya watumiaji wa magali hayo yanayotoa huduma za usafiri wa ndani ya mji huo.
Mwenyekiti huyo aliwataka kusimamisha zoezi hilo la ujengaji wa vibanda vya biashara zao kutokana na kile alichosema ugawaji ugawaji wa nafasi hauzingitia utarabu kutokana na viongozi wa machinga hao kupewa jukumu la kusimamia.
Mwanga aliongeza kuwa alifika eneo hilo kutokana na kusikia malalamiko ya baadhi ya machinga kulalakia kutotendewa haki wakati zoezi la ugawaji likiendelea kwakuwa wengi wao walijikuta wakiwekwa pembeni tofauti na walipokuwa kabla ujenzi huo haujaanza Augost 2012.
Alisema alipofika na kujionea kilichokuwa kikiendelea Stend hapo aliamua kumjulisha mkurugenzi hali halisi na hivyo kuamuliwa zoezi la ujenzi na uwekaji wa vibanda lisimamishwe na kamati ndogo iundwe ili ikutane na uongozi wa manispaa ili walijadili na kuliweka sawa swala hilo.
' Nimesimamisha ujezi usiendelee kwa sababu mtu akishajenga kumuondoa inakuwa ngumu, mimi na kamati yangu ya mipango miji na mazingira tutakutana na Meya na Mkurugenzi wa manispaa ili tulitatue swala hili kwa pamoja na kamati yao mapema iwezekanavyo ili Abiria waendele kupata mahitaji yao kama kawaida'', alisema Mwanga
kwa upande wao baadhi ya Machinga hao walisema viongozi wamejilimbikizia nafasi zaidi ya moja kwa kutumia majina tofauti mpaka ya wake zao huku sura nyingi mpya zikipenyezwa hata wakati staend hiyo kabla ya kuhamishwa hawakuwepo huku nafasi hizo zikibanwa kuwa ndogo na wao kujipendelea nafasi za mwanzo.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao wadogo wadogo Haji kulaya alisema mpangilio huo wa viongozi hauwezi kubadilishwa kutokana na ramani ya stand hiyo kubadilika kuwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo hali iliyofanya kuwe na mpangilio mpya katika ugawaji.
 ASKARI POLISI WAKISIMAMIA UBOMOAJI WA VIBANDA HIVYO
 baadhi ya wafanyabiashara wakiokota bidhaa zao zilizomwagika chini wakati wa kukusanya kuondoka kituoni hapo baada ya tangazo la serikali
 wengine wakibeba friji kuondoa shemu hiyo ya kituo cha daladala
kama kawaida baada ya tangazo kifuatacho ni utekelezaji hapa tingatinga likiwa kazini kubomoa vibanda vya wafanyabiasha katika eneo hilo la standi mjini dodoma
 mbao zikikusanywa baada ya kubomolewa
PICHA NA JOHN BANDA