Monday, July 15, 2013

STARS NA UGANDA WAINGIZA MILIONI 113/=.



Mrisho Ngasa, akijaribu kuwatoka mabeki wa Timu ya Uganda, wakati wa mcheo wao uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar.
***********************************
Mechi ya kwanza mchujo ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) iliyochezwa jana (Julai 13 mwaka huu) imeingiza sh. 113,268,000 kutokana na watazamaji 17,121.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 17,278,169.49 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.
Asilimia 15 ya uwanja sh. 13,227,108.98, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 17,636,145.30 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 4,409,036.33.
Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 52,908,435.91 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,645,421.80 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
*WAKATI HUO HUO TAIFA STARS KAMBINI TENA JULAI 4
Timu ya Taifa (Taifa Stars) imeondoka leo asubuhi (Julai 14 mwaka huu) kwenda Mwanza ambapo itapiga kambi ya siku kumi kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Uganda (The Cranes) kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeondoka kwa ndege ya PrecisionAir na itafikia hoteli ya La Kairo wakati mazoezi yatafanyika Uwanja wa CCM Kirumba kulingana na programu ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.
Wachezaji walioko katika kikosi hicho ni Juma Kaseja, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vincent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd na Haruni Chanongo.
Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Julai 26 na 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nelson Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala. Tarehe rasmi itapangwa na Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu vya Uganda (FUFA) siku kumi kabla ya mechi

No comments:

Post a Comment