Tuesday, July 23, 2013

LWAKATARE KWENDA INDIA KWA MATIBABU

Mkurugenzi wa ulinzi na usala wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wilfred lwakatare 

mahakama ya mkazi kisutu jijini dar es salaam imekubali kutoa kibali cha kwenda nje ya nchi kutibiwa  mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chadema wilifred lwakatare anayekabiliwa na shtaka la kula njama ya kutaka kumkamata na kumtesa mhariri wa gazeti la mwananchi denis msaky.

kibali hicho kimetolewa jana na hakimu aloyce katema baada ya wakili wa bwana lwakatare, nyaronyo kicheere kuwasilisha nyaraka za madaktari wa muhimbili zinazoonyesha matatizoi ya mgongo yanayomsumbua  mteja wake.

kicheere alidai kuwa lwakatare anaumwa na hivyo anahitaji kwenda kutibiwa  india na kuiomba mahakama kutoa kibali kwaajili ya kwenda india bwana lwakatare.

mahakama ilikubali ombi la wakili na hakimu  katemana alitoa kibali cha bwana lwakatare kwenda india kwa matibabu.

No comments:

Post a Comment