Obama akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Tanzania leo Jumatatu kwa
zara ya siku mbili, ikiwa ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake
barani Afrika akitokea nchini Afrika Kusini.
Obama ambaye ameambatana na mkewe Michelle Obama amepokelewa na mwenyeji
wake rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Salma Kikwete katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kisha kuelekea Ikulu
ya rais.
Rais wa Marekani akicheza muziki wa band wakati alipotua uwanjani
Rais Obama na mwenyeji wake wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya pamoja na
kisha Obama atafanya mazungumzo na waandishi wa habari kabla ya
kushiriki dhifa ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali hapo
baadaye Ikulu jijini Dar es Salaam.
Aidha hapo kesho Obama atatembelea kituo cha umeme cha Ubungo , baada ya
kuahidi kutoa dola za Marekani bilioni saba kusaidia mradi wa umeme
Barani Afrika.
Mpango huo wa serikali ya Marekani utazinduliwa kwanza katika nchi za
Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria na Tanzania ambazo wananchi
wake wanakumbwa na matatizo ya upatikanaji wa umeme.
Karibu Barack Obama kanga pamoja na vitenge vyenye picha ya Obama waliova wananchi wa waTanzania kumkaribisha Rais wa Marekani
Katika ziara yake Barani Afrika iliyoanzia nchini Senegal, Afrika kusini
na hatimaye nchini Tanzania Obama amaekuwa akisisitiza suala la
demokrasia ambapo ameeleza kuwa Afrika itakuwa na mustakabali mzuri kwa
kuwa na viongozi wanaopambana kuhakikisha raia wao wanakuwa na maisha
bora.
Katika ziara yake nchini Afrika Kusini , Obama hakusita kusifu jitihada
za kiongozi wa zamani na baba wa taifa hilo Nelson Mandela ambaye
ameeleza kuwa jitihada zake za ukombozi kwa raia wa taifa hilo
zilimsukuma kuingia katika siasa na hatimaye kuwa rais wa kwanza mweusi
nchini Marekani
No comments:
Post a Comment