Na John Banda, Dodoma .
Afisa Elimu Taaluma wa
manispaa ya Dodoma Suma Mwampulo amejiingiza katika mgogoro na waandishi wa
habari baada kuwafukuza wasifanye majukumu yao na kuwajibu majibu mabaya.
Hali hiyo ilijitokeza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo
walimu wanaofundisha masomo manne kwa Darasa la saba na kidato cha nne
iliyofanyika ukumbi wa Dodoma
sekondari.
Ofisa huyo alianza kufanya kazi ya kutoa
waandishi mmoja kwa mwingine katika ukumbi huo walipokuwa wameenda kusikiliza
malalamiko ya walimu waliokuwa wamegoma kuendelea na semina hiyo kutokana na
kutolipwa posho zao.
Suma aliwatoa nje waandishi hao huku akiwataka
kutorudi wala kufuatilia mararamiko ya walimu hao waliokuwa wakidai 125,000 kwa
kila mmoja huku akidai hiyo siyo habari hivyo wafuate mambo yao .
Kwa upande wao waandishi waliofika katika
ukumbi huo Hamida Ramadhan [TZ. Daima], Jonas Marios [Dayilnwes], Abdalla
Rashid [Zenji FM], Mariam Kasawa [Dodoma FM.] walisema kitendo cha Ofisa huyo
si cha kiungwana.
Walisema kitendo alichoonyesha Ofisa huyo ni
kujua wajibu wake, huku wakiongeza kuwa mtu anaeonyesha hofu kwa wanahabari
lazima atakuwa na tatizo kiutendaji ndiyo maana anajihami wakati wote.
Kwa upande wa walimu walisema wao hawawezi
kuendelea na Mafunzo hayo kutokana na kukosa Fedha za kujikimu, hali iliyowanya
wengi wao kulala wanne kwenye nyumba za kulala wageni.
Walimu waliongeza kuwa tangu mwanzo wa semina
hiyo waliahidiwa kupewa tsh. 25,000 kwa siku tano zinazoishia Ijumaa lakini
baada ya kuhoji kuhusu kuchelewa kwa mailipo hayo walisema wanatishiwa.
Huku wakisisitiza majina yao kutitajwa Gazetini walitanabaisha kuwa
wanaogopa kujulikana kwani Ofisa Taaruma huyo akiambiwa ukweli kuhusu masrahi
ya walimu huwa anamtafuta aliyeanzisha na kumwandikia Barua za kumhamishia
kijijini zaidi
''Sikia mwandishi mimi naitwa mwl, wa shule
jina tunalo lakini sitaki kutajwa gazetini, huyu Suma huwa akiambiwa ukweli
anafuatilia akijua ni nani unashtukia Barua ya uhamisho kijijini utajijua
mwenyewe'', alisema mmoja wa walimu hao
Semina hiyo iliyoanza Jumatatu wiki hii
ilikuwa inalenga kupandisha kiwango cha ufaulu kwa Darasa la saba na kidato cha
4 ambayo matokeo yake yamekuwa yakiporomoka mwaka hadi mwaka.
No comments:
Post a Comment