Monday, July 29, 2013

MABANGO YA TIGO NA VODA DODOMA KUSHUSHWA CHINI NA HALMASHAURI YA DODOMA.


MADIWANI wa halimashauri ya manispaa ya Dodoma wamemtaka muwekezaji
anayeshughurikia mabango ya matangazo yote ya kampuni za simu
yanayowekwa kwenye taa  za barabarani ayashusha ndani ya siku saba.

Madiwani hao walifikia makubaliano ya kuchukua hatua hiyo ya kumuondoa
mwewekezaji huyo kwenye Baraza  la kawaida la madiwani lililokutana
ili kujadili kwa kina maswala mbalimbali ambayo yamekuwa yamekuwa
kikwazo katika mapato halimashauri yao.




Madiwani wa Halimashauri ya manispaa ya Dodoma wakiwa katika ukumbi wao wa mikutano wakifuatilia hoja mbalimbali kwa umakini wakati walipokuwa kwenye mkutano wao wa kawaida juzi ambapo waliazimia kuyashusha mabango yote ya Voda, Tigo na Artel kwenye taa za barabarani.



Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini DKT David Malole akifafanua jambo alipokuwa akiongea na madiwani kwaenye mkutano wao wa kawaida.



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma akizungumza jambo na madiwani waliokuwa kwenye Baraza maarum kujadili hoja maarum na kuzipatia majibu.


wataalamu wa fani mbalimbali wa manispaa hiyo wakifuatilia agizo la madiwani kwa makini sana

No comments:

Post a Comment