Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere .
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo jioni amewaongoza watanzania kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere .
Makamu wa Rais, Viongozi wengine waliofika kupokea Miili hiyo, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na mkewe, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.
Askari wakishusha majeneza yenye miili ya askari wenzao waliofariki dunia huko Darfur.
Askari wa Jeshi wakijipanga kupokea miili hiyo kwa heshima.
Nape Nnauye na Ridhiwan Kikwete, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria.
Msafara wa magari ya Jeshi yaliyobeba miili hiyo ukianza safari ya kuelekea Lugalo
No comments:
Post a Comment