Wednesday, July 31, 2013

POLISI MKOANI DODOMA WAKAMATA MITAMBO YA KUTENGENEZA GONGO

 Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akionyesha mitambo ya gongo iliyokamatwa.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya mitambo ya kutengenezea pombe Haramu aina ya Gongo waliyoikamata hivi kalibuni katika wilaya za mpwapwa na kongwa, na kumshikilia Taita Rashid pamoja na gongo lita 600.

[PICHA NA JOHN BANDA]


 

MAANDALIZI YA SIKUKUU YA NANE NANE MKOANI DODOMA YAMEPAMBA MOTO



Mafundi wakichekecha mchanga walipokuwa katika hatua za mwisho za umaliziaji wa ujenzi wa jengo la Bank ya uwekezaji Tanzania [T I B] lililopo ndani ya viwanja vya nanenae ili kujiandaa na maonyesho ya wakulima yanayotarajiwa kuanza Agosti mosi na kutimishwa agosti 8 mwaka huu mkoani Dodoma.


huu ni ujenzi wa banda la bank ya TIB huduma inapatika muda wote ndani ya viwanja vya nane nane mkoani dodoma


Fundi akipaka rangi moja ya nguzo zilizopo pembezoni mwa jukwaa kuu la viongozi litakalotumika kwa ajili ya maegesho ya magali, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maonyesho ya wakulima maarufu kama nanenane yatakayoadhimishwa kitaifa Nzuguni Mkoani Dodoma.  
(PICHA NA JOHN BANDA)

Tuesday, July 30, 2013

CPC DODOMA WAPATA VIONGOZI WAPYA.HONGERENI SANA MAJEMBE MAPYA YA CPC



Katibu Mkuu Mpya wa Chama cah waandishi wa habari mkoa wa Dodoma [cpc] Israel Mgusi  akitoa  shukurani zake baada ya kuchaguliwa.





Mwanasheria wa kujitegemea Elias Machibya akiwaelekeza waandishi wa habari mkoa wa Dodoma utaratibu wa kisheria kuhusu uchaguzi kabla ya upigwaji wa kura.



Tabasamu la viongozi wapya waliochaguliwa kuongoza chama cha waandishi wa habari mkoa wa Dodoma kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo Joyce kasiki alitetea kiti chake cha uenyekiti, na Israel Mgusi kushika nafasi ya ukatibu mkuu.

                                                         viongozi waliomaliza muda wake
PICHA NA JOHN BANDA