Na John Banda, Dodoma
WAKAZI wa Kata za
Kikuyu Kusini na Kilimani mkoani Dodoma wameandamana kupinga amri iliyotolewa
na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika
eneo hilo ndani ya siku saba.
Wakazi hao
walioandamana kutoka Kikuyu hadi Viwanja vya Nyerere Square katikati ya mji
wakimtaka mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi kuzungumza nao.
Maandamano hayo
yalisindikizwa na ulinzi wa polisi hadi katika viwanja hivyo huku wakazi hao
wakiwa wameshikilia mabango yenye jumbe mbalimbali.
Wakazi hao wakiwa
wanaimba nyimbo huku wakiinua mabango yao juu yenye ujumbe kama Cda ni zaidi ya
Alshababi, CCM mnaiona bomoabomoa, Cda ni zaidi ya Nduli Idd Aminini Dada na
lingine likisomeka Hata wanyama hupewa hifadhi.
Wakizunguza na
waandishi wa habari katika viwanja hivyo wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa baadhi
ya wananchi na viongozi wao wa mitaa walidai kuwa lengo la maandamano hayo ni
kufikisha kilio chao kwa serikali ya mkoa.
Andrew Mdumi
mwenyekiti wa mtaa wa Mkalama ambao ni sehemu ya eneo linalotakiwa kuvunjwa
alisema kuwa wameamua kufanya maandamano hayo mara baada ya kupewa amri ya
kuondoka katika eneo wanaloishi kwa kipindi kirefu.
Mdumi alisema, kuwa
Mamlaka ya ustawishi Makao makuu imekuwa ikiwapatia namba kila wakati na kudai
kuwa itakuja kuwapimia lakini katika hali ya kushangaza imewapa amri ya
kuondoka ndani ya siku saba kwa madai kuwa wamevamia katika eneo hilo ambalo
lilikuwewa limetengwa kwajili ya bustani za mbogamboga na matunda.
Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana
katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya
ustawishaji makao makuu [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na
misingi ya wakazi hao.
Moja ya
bango lenye ujumbe lilotumika katika maandamano hayo
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akipaza sauti ya matumaini kwa wakazi wa Kata ya kikuyu kusini walioandamana kupinga Bomoabomoa ya CDA waliokuwa wamepanga kubomoa nyumba na misingi katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment