Thursday, September 12, 2013

WANANCHI WA IYUMBU WAKUBALI MATAKWA YA CDA.



Na John Banda, Dodoma
WANANCHI wa kata ya iyumbu manipaa ya Dodoma wamekubali kwa Shingo upande matakwa ya Mamlaka ya ustawishaji makao makuu [CDA] ya kutakiwa kutopewa viwanja vya bure tofauti na makubaliano ya awali.
Hatua ya wananchi hao  kukubali matakwa hayo ilikuja katika mkutano wa kijiji hicho ulioitishwa na viongozi waliomtaka Kaimu Mkurugenzi wa CDA Paskasi Muragili kufika na kujibu malalamiko ya wananchi hao.
Mkazi wa kijiji hicho Rafael Wiliam alisema hakuna mtu wa kijiji hicho na hata manispaa nzima aliye na imani na CDA kutokana na mamraka hiyo kuingia katika mashamba na makazi ya watu na wanapomaliza kupima wenye maeneo wanakosa haki.
Mkazi huyo alisema CDA kabla ya kupima katika kijiji hicho mwaka jana 2012 kwanza walikubaliana kwenye vikao kuwa baada ya kupima wangewapa viwanja 2 kimoja wangelipia kingine kingekuwa sehemu ya fidia na makubaliano hayo ndiyo yaliwafanya walikubali zoezi hilo.
Wiliam aliongeza kuwa walianza kushangaa walipopewa fidia bila kuambiwa utaratibu wa viwanja walivyokubaliana ukoje lakini wakajipa moyo kuwa wasubili kitu cha ajabu zaidi ni baada ya muda kutangaziwa na mamraka hiyo kuwa wanatakiwa kulipia 94,000 ya fomu na kutakiwa kulipia viwanja 4200 kwa Squre mita 1.
“ Tunashangaa sana hawa jamaa ni wafanya biashara wenye kutaka faida mara dufu maana wao walitulipa fidia ya 600 kwa Squre mita 1, na leo wameongeza 3600 kama faida mwananchi wa kijijini atazitoa wapi wakati walilipwa kidogo na hata mlo ni mmoja kwa siku? Alihoji William.
Kwa upande wake Diwani wa Kijiji hicho Hezeron Kudugwa alisema chanzo kikubwa cha CDA kulaumiwa na wananchi ni kitendo cha mamraka hiyo kufika site wanamshirikisha mwenye eneo kwa hatua zote wakati wa uthamin lakini baada ya kumaliza na kuondoka hawamjulishi eneo lake linaukubwa kiasi gani.
Kudugwa alisema ni vigumu sana mamraka hiyo kujiondoa kwenye lawama mpaka watakaporekebisha hisia za kudhurumiwa kutokana na vipimo vya  maeneo hayo kuwa siri ya wapimaji wa CDA pekee.
Akiongea kwenye mkutano huo kaimu Mkurugenzi wa CDA Paskasi Muragili aliwataka wanakijiji hao kupunguza jazba na kuukubali mpango huo wa kulipia kwa kiasi hicho bila ya mabadiliko yoyote kwa sababu ya kutovunja mahusiano kati yao.
Aliongeza kuwa kuendelea kung’ang’ania wapewe viwanja hivyo bure ni kinyume cha sheria na kama wakiwa na msimamo huo hata hivyo watanyang’anywa na mamraka na kuuzwa kwa wengine.
“Kubalini mtalipia kwa muda wa mwaka mmoja unaonza mei 2013 mpaka Aprl 31 2014 kama mtu atashindwa atafute ndugu jamaa au rafiki wakubaliane aje alipie bila shaka kwa utamaduni wetu atakupa asante hata kama utamuachia kiwanja hicho’’, alikazia Muragili
Aidha Muragili alisema wao walilipa 600 na kwa ukubwa huohuo kuuza 4200 ni kutokana na Gharama za uthamin, miundo mbinu ya maji na Barabara likiwemo Deni la benki zaidi ya 5 bil ambalo CDA ilikopa kulipia fidia hivyo lazima kulipa hivyo na kwa mjini ni 5000 na 7000 kwa Squre 1
Jumla ya viwanja 1200 vilipimwa na Mamraka hiyo mwaka 2012 katika eneo linaloitwa Iyumbu North ndani ya kijiji hicho kilichopo kilometa 12 toka Dodoma mjini ambapo wananchi hao wamezipongeza Shirika la Nyumba [NHC], LAPF na CCM wanaotaka kujenga majengo yao kijijini hapo kutokana na kuthamin, kupima na kulipa vizuri.


Kaimu Mkurugenzi wa Mamraka ya ustawishaji makao makuu Paskasi Muragili akijairibu kuwapoza wananchi wa kijiji cha iyumbu kuhusu kero ya aridhi.


Maafisa wa CDA walioongozana na Kaimu Mkurugenzi Paskasi Muragili wakiwa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha iyumbu manipaa ya Dodoma walipofika kusikiliza kero zao



 Wanchi wa kijiji hicho wakiwa kwenye mkutano huo ulioamuliwa wananchi walipe 4200 kwa CDA tofauti na fidia ya 600 kwa Squere walizolipwa awali.
PICHA NA JOHN BANDA

No comments:

Post a Comment