Ni baada ya Kinana kupeleka neema ya
wakulima wa pamba(soko na bei).
~. Ujenzi wa viwanda Shinyanga wawapa homa
~. Ajira kwa vijana kuwakosesha Chadema waandamanaji.
~. Waishia kumparamia balozi wa China
~. Kinana: tuna deni la kuwatumikia wananchi sio kulumbana.
Kasi ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha 2010/2015
imeibua kiwewe kwa vyama vya upinzani hasa Chadema. Kiwewe hicho
kimedhihirishwa na shutuma za Chama hicho kwa balozi wa China nchini kwa uamuzi
wa nchi hiyo kuwekeza kwenye viwanda vya pamba na mazao yatokanayo na mifugo
kwa mkoa wa Shinyanga.
Katika mkutano wa Chadema na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana,
Chadema walidai kitendo cha Balozi wa China Dk. Lu Youqing kushiriki katika
mkutano wa hadhara wa CCM mjini Shinyanga ni cha utovu wa nidhamu, uvunjifu wa
sheria hoja ambazo hazina mashiko.
Hata hivyo Katibu wa NEC ya CCM itikadi na uenezi Ndg. Nape Nnauye akiongea na
waandishi wa habari kijijini Mwandoya, wilayani Meatu mkoa wa Simiyu kwenye
ziara ya Katibu mkuu wa CCM mkoani humo aliwataka watanzania na wanakanda ya
ziwa kuzipuuza shutuma hizo dhidi ya balozi wa China na akawataka waendelee
kuunga mkono juhudi za CCM za kutekeleza ilani yake ya uchaguzi.
"tatizo la hawa Chadema wamezoea kufanya harakati zao kwa kutumia matatizo
ya watu, sasa leo juhudi za CCM kutatua tatizo la bei ya pamba na soko lake
inawanyang'anya mtaji wao muhimu sana ndo maana wanapiga kelele. Lakini pia
tatizo la ajira kwa vijana wao walikua wanalitumia kama mtaji wa kupata
waandamanaji, sasa vijana wakipata ajira kwenye viwanda hivi ambavyo vitaanza
kazi Desemba mwaka huu, watakosa waandamanaji ndio chanzo cha kelele zote
hizi" alisisitiza Nape
Nape alisisitiza kuwa vyama vyote vya siasa vina vyama rafiki kutoka nchi
mbalimbali duniani, lakin tofauti inakuja kwenye aina ya urafiki husika, na
kutoa mfano wa tofauti ya urafiki kati ya Chama Cha Kikomunisti cha China na
CCM kuwa umelenga katika shughuli za maendeleo, lakini kwa upande wa Chadema ni
tofauti.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Kinana amekuwa akisisitiza mara kadhaa kuwa CCM ina
deni kubwa la kuwatumikia wananchi katika kutimiza ahadi zao kwa wananchi
walizozitoa kupitia ilani ya uchaguzi ambayo watanzania waliichagua mwaka 2010
na ahadi mbalimbali za wagombea wa CCM.
"sisi CCM tuna kazi ya kuwatumikia wananchi,kutimiza ahadi zetu kwao na
sio kulumbana na wapinzani. Na hii ndio tofauti ya chama kilicho madarakani na
vyama vya upinzani, wakati wao kila kukicha wanatafakari wazungumze nini sisi
tunahangaika kuwatumikia wananchi waliotupa dhamana ya kuongoza nchi yetu.
No comments:
Post a Comment