BIHAR, Jharkhand, India |
Mahakama Kuu ya Ranchi nchini India imetoa hukumu
kwa,
Lalu Prasad (66), pamoja na washtakiwa wenzake 44 kwenda jela baada ya
kupatikana na hatia ya rushwa wakati alipokuwa waziri mkuu wa Bihar.
Kesi
hiyo iliyovuta hisia za watu wengi Lalu alipatikana na hatia ya
matumizi mabaya ya Rupia 37 crore alipokuwa waziri mkuu miaka 17
iliyopita. Hata hivyo hukumu hiyo itatangazwa siku ya Alhamisi kupitia video katika ukumbi wa mahakama hiyo.
Pia
alipatikana na kashfa kubwa wakati akiwa kama mtumishi wa serikali
kushindwa kuzuia matumizi mabaya ya fedha wakati akiwa waziri mkuu kiasi
cha Rupia 950 crores zilizotumika kulipia bili za hewa katika matumizi
ya madawa na chakula cha mifugo. Kufuatia hukumu hiyo Lalu amepoteza sifa ya kuwa mwanachama wa bunge, kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama Kuu hivi karibuni.
Washtakiwa wengine ni pamoja na waziri wa zamani
Waziri
Mkuu wa zamani Mishra Jagannath pia alipatikana na hatia katika
mahakama hiyo ya Juu kabisa, pamoja na wanasiasa wengine sita, wawili
ambao ni wa chama tawala cha Janata Dal-Muungano.
No comments:
Post a Comment