BAADA
ya warembo hao kukamatwa ilielezwa kuwa walikuwa wakigoma kueleza mzigo
huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa
upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa
wakieleza ukweli wataachiwa.
Chanzo
hicho kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao
wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema
aliyewatuma.
“Unajua Sauzi (Afrika Kusini)
huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya. Jamaa (polisi) wana kila
aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.
“Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.
“Kwanza utaanzia kwenye chumba
kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi
ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani
hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.
“Wakishakuingiza mle ndipo
utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung’ata mwili mzima,
zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.
“Kama bado ukijifanya mbishi
au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja
ndogo kwenye waya wa umeme.
“Si unajua tena waya wenye
umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya
kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea.
“Kinachofuata ni mtu kupigwa shoti kali ya umeme ambapo lazima utasema tu.
“Hicho ndicho kilichowapata akina Masogange kama wanavyofanyiwa Wabongo wengine wanaokamatwa Mitaa ya Rissik hapa Johannesburg.
“Baada ya mateso hayo,
waliwataja waliowatuma mzigo huo wa unga aina ya crystal methamphetamine
wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8,” kilisema chanzo hicho
ambacho ni Mbongo ambaye kwa sasa ni mkazi wa Mtaa wa Rissik,
Johannesburg, wanapoishi Wabongo kwa kuungaunga aliyewahi kukumbwa na
mkasa kama huo.
Habari za ndani zilidai kuwa
baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao waliwataja watu wawili
waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni mtoto wa kigogo ambaye
ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina lipo).
Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wa
mkubwa ni mjanja wa mjini ambaye alihusika kushughulikia kusafirisha
mwili wa msanii Albert Mangweha ‘Ngwea’ aliyefia Johannesburg Juni,
mwaka huu.
Ilivuja kuwa mwingine
aliyetajwa na akina Masogange ni mfanyabiashara maarufu Bongo
anayesafiri nje mara kwa mara huku jina la ‘mtoto wa mjini’ Mangunga
likitajwa zaidi hata na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George
Mwakyembe.
Kamanda wa Kitengo cha Kuzuia
na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kupewa majina
hayo lakini akaliomba gazeti hili kutoyachapisha kwa sasa kuepuka
kuvuruga ushahidi.
Baada ya polisi wa upelelezi
na wale wa kimataifa (Interpol) kujiridhisha na maelezo ya mabinti hao,
walipandishwa kizimbani kwa mara ya pili Agosti 19, mwaka huu chini ya
ulinzi mkali kama ule ‘anaowekewaga’ Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anapofikishwa kwenye mahakama
mbalimbali nchini kwa kesi zake za madai ya uchochezi.
Habari kutoka Sauzi zilieleza
kuwa akina Masogange walipandishwa tena kizimbani hivi karibuni ambapo
tayari kesi yao imeanza kuunguruma ikielezwa kuwa endapo watakutwa na
hatia watakula mvua ya kifungo si chini ya miaka 10 kwa sheria za nchi
hiyo.
Masogange na Mellisa walinaswa nchini humo Julai 5, mwaka huu wakiwa na mabegi sita yaliyokuwa na mzigo huo wa unga
No comments:
Post a Comment