Na John
Banda, Chamwino
WAKAZI wa
kata ya Segara Wilayani Chamwino mkoani Dodoma wamelalamikia kukosekana kwa
huduma ya mawasiliano hali inayowafanya kukosa huduma za msingi kwa wakati
ikiwemo kuuza mazao kwa bei yahasara.
Wakazi hao
waliitoa kauli hiyo katika kijiji cha Malechala walipokuwa kwenye Tambiko la
kimila lilihudhuliwa na makabila mbalimbali yaliyoongozwa na Wanguu toka mkoani
Tanga lililohudhuriwa na watu zaidi ya 400 na kufanyika katika himaya ya Fundi
Shabani Waziri mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mmoja wa
wakazi wa kijiji hicho Asha Mohamed alisema kumekuwa na kelo ya
ukosefu wa mitandao ya mawasiliano tangu ilipoanzishwa hapa nchini hali ambayo
imekuwa ikiwasababishia kukosa kila huduma za kijamii kwa wakati.
Alisema
kutokana na kata hiyo kuwa mbali na makao makuu ya wilaya hiyo ya Chamwino
wamekuwa wakipata taabu ya utoaji wa taarifa za matukio mbalimbali zikiwemo za
ajali, ujambazi, wizi, wagonjwa wanaohitaji huduma za haraka pia wameshindwa
kujua wakati mzuri bei za mazao.
Mwanamama ambaye hakufahamika jina akiwa ndani ya shimo huku
akielekezewa Damu ya mbuzi aliyekatwa shingo wakati alipokuwa akipata moja ya
tiba zinazotolewa nyumbani kwa mzee Shabani Waziri aliyeamua kuijenga nyumba
hiyo katikati ya poli na umbali wa kuingia kijiji cha Malecela km 2 .
Kiongozi wa waganga wa tiba za jadi Fundi Shabani
Waziri akimshika mmoja wa waganga waliohuzuria tambiko hilo kama ishara ya
salamu zinazotumika wakati wa tambiko.
Mgeni
Rasmi katika tambiko hilo Fundi mkuu wa waganga wa tiba za jadi Sangali Chambo
akimuwekea mkono Kiongozi wa waganga hao Shabani Waziri kama kielelezo
cha salamu za heshima wakati wa tambiko hilo lilifanyika katika himaya yake
kwenye nyumba iliyopo umbali wa zaidi ya km 2 toka kijiji cha Malecela.
No comments:
Post a Comment