Wakati
mapambano bado yanaendelea dhidi ya wanamgambo wachache wa al Shabaab
waliobaki ndani ya Westgate Mall, maofisa wa Kenya wamesema angalau al
Shabaab watatu wameuawa katika harakati za kuokoa mateka
Taarifa
zinasema mmoja wa magaidi hao ni mwanamke wa kizungu. Inaaminika kuwa
mwanamke huyo aliyetajwa ni Samantha Lewthwaite, al-maarufu kama “White
Widow” au “Mjane Mweupe” au “Mjane wa Kizungu” kwa Kiswahili. Samantha
anaripotiwa kuwa ndiye kiongozi wa kundi hilo lililofanya mashambulizi.
Inasemekana kwamba kati ya magaidi waliouawa, mmoja wao ni mwanamke wa kizungu lakini bado haijajulikana kama ni Samantha.
Kwa
mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, mume wa Samantha alikua
mpiga mabomu wa kujitoa mhanga (suicide bomber) anayeitwa Germaine
Lindsay ambaye baada ya kusilimu alitumia jina la Abdullah Shaheed
Jamal.
Abdullah
Jamal alikua ni mmoja wa magaidi wenye asili ya Uingereza waliopiga
mabomu ya kujitoa mhanga katika treni tatu na kuua watu 56 nchini
uingereza Julai 7, 2005 ambao unajulikana duniani kama “Ugaidi wa 7/7″
No comments:
Post a Comment