Tuesday, September 3, 2013

TRAFIC FEKI ALIKUWA NI MFUNGWA NYAMPALA WA GEREZA KISANGA KABLA YA 'UTRAFIC FEKI'


Umesikia hii??????, Huyu askari wa Usalama Barabarani yaani 'Trafic Fek', aliyekamatwa Agosti 8, mwaka huu maeneo ya Kinyerezi Tabata, akiendelea kutekeleza majukumu yake ya kazi zake za kila siku aliyoamua kujiajili nayo, amegundulika kuwa alikuwa ni Mfungwa wa Gereza la Kisanga kabla ya kukamatwa kwa makosa hayo ya kugushi na kujifanya askari wa usalama Barabarani.

Askari huyo baada ya kukamatwa alifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Sitaki Shari Ukonga, na baadaye kwenda kupekuliwa nyumbani kwake, ambapo aliwekwa Mahabusu na hatimaye kupelekwa Gereza la Ukonga ambako yupo hadi sasa.

Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Trafic huyo Feki, wakati akiwa mahabusu katika Gereza hilo, baada ya kuchunguzwa na kufuatiliwa amegundulika kuwa alikuwa ni mfungwa katika Gereza la Kisanga alikokuwa akitumikia kifungo cha kiaka 30, ambako alikuwa amepewa Unyampala yaani kiongozi na mlinzi wa wafungwa wenzake baada ya kuonekana kuwa ni Mtiifu na mpole. 

Mtonyaji wa habari hizi, anatonya kuwa, baada ya kufuatilia Faili lake la Trafic huyo na kugundulika kuwa tayari alikwisha idhalilisha Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kutoroka wakati akiwa ni mfungwa wa miaka 30, sasa anatarajia kurejeshwa Gereza la Kisanga ili akasomewe shitaka jipya la kutoroka gerezani hapo na kisha kuendelea na kifungo chake cha miaka 30, kisha kuhukumiwa kwa kosa la kutoroka na baada ya hapo ndipo arejeshwe kuendelea kushikiliwa kwa kosa lake la Utrafic feki

No comments:

Post a Comment