Tuesday, October 1, 2013

MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA AFUTIWA KESI YA UCHOCHEZI.

Kesi ya Uchochezi iliyokuwa ikimkabili Mbunge Lema imefutwa!

Upande wa mashitaka, Jamhuri imeiomba Mahakama kufuta kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili Mhe. Lema. Hii ni ile kesi ya kudaiwa kuchochea vurugu Chuo cha Uhasibu Arusha. 
BAADA YA KUFUTWA KESI HIYO LEMA ANASEMA:
 "Nimeshinda kesi tena! Kwa kweli Mungu anatupenda sana na tutaendelea kupambana kutafuta haki bila hofu. Miili yetu na nafsi zetu zimepoteza maumivu kwa sababu ya mateso yaliyojaa uongi na hila. Hata hivyo tutaendelea na kelele za kupigania haki bila kurudi nyuma huku uvumilivu ukiwa nguzo yetu kuu" alisema Mbunge Lema ,
 katika viwanja vya Mahakama Kuu Arusha mara baada ya kushinda kesi dhidi yake na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo zikihusisha kilichodaiwa kuwa uchochezi kwa wanafunzi wa Uhasibu Arusha wamzomee Mulongo na kufanya fujo... Kesi hiyo imefutiliwa mbali baada ya washitaki kuomba hivyo pamoja na kwamba leo ndio ilikuwa siku ya kuanza kusikiliza ushahidi wa Mkuu wa Mkoa, Dean of Students, Makamu Mkuu wa Chuo na Maofisa wa Polisi wakiongozwa na OCD Muroto

No comments:

Post a Comment