Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema NChimbi amewataka waratibu wa mapambano dhidi ya UKIMWI kutoka wilaya za Mikoa ya Dodoma na Singida kuitazama mikoa ya kanda ya kati hususani dodoma na Singida kwa jicho la kipekee na kuongeza nguvu zaidi katika uratibu wa mapambano dhidi ya ukimwi na unyanyasaji/ukatili wa kijinsia.
Dr. Nchimbi alibainisha kuwa sababu za kijiografia, maendeleo ya miundombinu na kwa sasa Dodoma ndio kama Mkoa mama wa vyuo vikuu na elimu ya juu kwa kuwa na chuo kikuu kikuba Afrika Mashariki na Kati (UDOM) vyote hivi ni vivutio ama vichocheo vilivyoongedza idadi ya watu na mwingiliano hivyo kuifanya mikoa hii miwili kuwa eneo hatarishi zaidi kwa maambukizi ya VVU/UKIMWI.
Mkuu w Mkoa aliyasema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya utumiaji wa zana ya kukusanya takwimu za jinsia, VVU na UKIMWI kwa waratibu wamapambano dhidi ya UKIMWI kutoka Wilaya za mikoa ya DDodoma na Singida.
Akizungumzia masuala ya jinsia, VVU na UKIMWI Dr. Nchimbi alibainisha takwimu zinaonesha Dodoma na Singida ni miongoni mwa mikoaambayo inaukatili wa kijinsia kwa kiasi kikubwa. Taarifa ya ofisi ya takwimu ya serikali 2010 inaonesha kuwa hali ya ukatili wa kingono na mabavu kwa nchi yetu ni asilimia33 lakini kwa Mkoa waDodoma imefikia asilimia 50 wakati Singida ni asilimia 46. Pia kwa ukatili huo wa kingono, wanawake wawili (2) kati ya wanawake kumi (10) wanafanyiwa ukatili huo.
Dr. Nchimbi alisema kuwa hali hii ya ukatili ni kubwa na inasababisha madhara ya kiafya kwa wanawake na wasichana na pia huvunja minyororo ya haki za binaadamu hivyo kuwataka waratibu hao wasiyafumbie macho mambo hayo bali waongeze nguvu kupinga unyanyasaji na ukatili huo. Aindha wartibu pia wasifumbiemacho viashiria na mazingira yote hatarishi ya nayoweaa kusababisha ongezeko la VVU/UKIMWI akitolea mfano matendo maovu yanayoshamiri kwenye kambi za starehe na klabu za usiku ambapo wateja wakubwa ni vijana na wanafunzi wa vyuo.
Kwa upandewake mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Dodoma Bi. Audry Njelekela alieleza kuwa changamoto za kupambanana VVU/UKIMWI na unyanyasaji/ukatili wa kijinsia na kingono kwenye mikoa ya Dodoma na Singida zinafanana na hivyo kuahidi kuongeza nguvu za kupambana na vitendo hivyo huku wakiongeza ushirikiano.
Aidha amesema matatizo ya UKIMWI na unyanyasaji/ukatili wa kijinsia na kingono ni tatizo mtambuka na hivyo ameita wadau wengi zaidi na jamii kwa ujumla kuingia kaika mapambano haya.
Mkuu wa Mko wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi
(katikati) akikazia jambo wakati akifungua mafunzo ya waratibu wa mapambano ya
UKIMWI kutoka wilaya za mikoa ya Dodoma na Singida, mafunzo hayo
yalifanyika jana mjini Dodoma, kushoto ni Afisa jinsia kutoka TACAIDS makao
makuu na kulia ni mratibu wa TACAIDS mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya wratibu wa kupambana na UKIMWI kutoka mikoa ya Dodoma na Singida wakiorodhesha maelekezo ya mkuu wa mkoa waDodoma Dr. Rehema Nchimbi (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya utumiaji zana ya kukusanya takwimu za jinsia, VVU na UKIMWI yaliyofanyika jana mjini humo.
Picha yapamoja kati ya Mkuu wa mkoawa
Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (katikati waliokmaa) na waatibu wa mapambano dhidi ya
UKIMWI kutoka mikoa ya Dodoma na Sigida mara baada ya hafla ya ufunguzi
wa mafunzo kwa waratibu hao juu ya utumiaji zana ya kukusanya takwimu za
jinsia,VVU na UKIMWI, mafunzo hayo yalifanyika jana mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment