Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Mweneyekiti wa CCM, Rais
Jakaya Kikwete alipowasili Makao Makuu ya CCM, Jengo la White House,
mjini Dodoma, kufunga mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za
wilaya na mikoa, jana, Oktoba 24, Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Philip Mangula.
Mweneyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akionyesha kuwa mwenye furaha, alipowasili
ukumbini kufunga mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za
wilaya na mikoa, jana, Oktoba 24, 2013 mjini Dodoma. Mafunzo hayo
yaliyokuwa ya siku nne yalifunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM,
Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Philip Mangula na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana.
Ukumbi
ukilipuka kwa mbinje, nderemo na vifijo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete alipowasili ukumbini, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma kufunga
mafunzo ya watendaji na viongozi wa CCM.
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, baada ya
kuwasilini ukumbini na kulakiwa kwa shangwe na wahitimu wa mafunzo kwa
wa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya nchini mjini
Dodoma, jana, Oktoba 24, 2013.
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya
watendaji na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa hapa nchini, mjini
Dodoma , jana , Oktoba 25, 2013. Kushoto ni Kinana na Kulia ni Mangula.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akizungumza namna
mafunzo hayo yalivyoandaliwa na Idara yake ya Itikadi na Uenezi na
kumalizika kwa mafanikio makubwa.
Baadhi ya viongozi wa Jumuia na Sekretarieti wakiwa ukumbini
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akitazama bango jipya la picha za
wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, baada ya mabango hayo kugawiwa kwa
washiriki wa mafunzo hayo ukumbini, wakati wa kufungwa mafunzo hayo.
Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye akihamasisha baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kifunga mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment