Na John Banda, Dodoma
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi amewataka madereva
wa magari ya Abiria na mizigo wanaopitia mkoa huo kuacha kutumia kilevi
chochote ikiwemo viroba wanapokuwa Barabarani la sivyo kufutiwa Leseni zao.
Mkuu huyo wa mkoa alitoa kauri hiyo siku ya usalama
Barabarani iliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma juzi.
Nchimbi alisema ulevi kwa madereva hao umekuwa
ukiwasababishia kuwa wazembe barabarani pindi wanapokuwa wakiendesha magali ya
abiria kwa maana ya mabasi na maroli ya mizigo na huwa ni chanzo cha ajali za
mara kwa mara.
Dr huyo wa Farsafa alisema ana taarifa za kutosha za ulevi
kwa baadhi ya madereva hao na hivyo atatumia jeshi la polisi kuwanasa na
kuwafutia leseni zao.
Aliongeza kuwa mbinu watakayotumia jeshi la polisi ni
kuwapima madereva wote wanaoingia na kutoka ndani ya mkoa wa Dodoma kwa
kipimo maalumu cha kung’amua ulevi na atakaegundulika kuendesha akiwa amekunywa
pombe au aina yoyote ya kilevi ikiwemo viroba atafutiwa leseni.
‘’Hivi sasa mkoa wetu unapoelekea kuwa jiji tunatakiwa pia
kuwa mfano wa kuigwa na mikoa mingine kuhusu udhibiti wa madereva walevi, hivyo
Dereva yoyote ili awe salama ahakikishe hajihusishi na ulevi ili aweze kupita
mkoa huu akiwa salama la sivyo apitie juu ama kama kuna njia ya kuzunguka apite
huko’’, alisema Dr. Chimbi
Aidha alisema zoezi hilo la kupima madereva walevi litaanzia
kwa wale wa Daladala na Bodaboda ambao wamekuwa wakinyonya viroba hata
wanapokuwa wanaendesha abiria wao bila kujali, aliwaagiza polisi kufavamia
maeneo yote wanakopakilia na kuhakikisha wanawapima hapo hapo na atakaebainika
uzi ni uleule wa kufutiwa leseni.
No comments:
Post a Comment