Na John Banda, Dodoma
MWANAMKE wa mwanajeshi aomba msaada kwa
wasamalia wema ili aweze kuwahudumia watoto wake kwa chakula mavazi na elimu
kutokana na ugumu wa maisha kiasi cha kushindwa kupata hata lishe ya kuwapa
mapacha watatu aliojifungua kinyume na matarajio yake.
Mwanamke huyo Rehema Khamis [30] mkazi
wa mkalama kata ya makulu manispaa ya Dodoma aliomba msaada huo baada ya kuona
toka ajifungue watoto hao watatu imefika wakati ameshindwa kuwapatia hata uji
wenye lishe huku mshahara wa Mumewe ukiishia kwenye madeni.
Rehema alisema alijifungua watoto
hao wa kiume wawili na wa kike mmoja Hassan, Husen na Hasanati katika hospitali
ya Rufaa ya Dodoma na sasa wanakaribia kuwa na umri wa mwaka mmoja aliowachisha
kunyonya wakiwa na miezi 7 kutokana na kukosekana maziwa.
Alisema hakutarajia kupata watoto
watatukwa mpigo kutokana na tayali alishakuwa na wengine wawili hivyo alijua
akipata mmoja angepumzika kuzaa ili ajipe nafasi ya kuwalea, hivyo kutokana na
watoto hao kuhitaji chakula, mavazi na hata elimu kwa hao wakubwa imekuwa ni
sababu ya kuhitaji msaada.
‘’Watu wa kada mbalimbali wamekuwa
wakifika kuwaona watoto hawa lakini ni kama uwanja wa \maonyesho na kutaka
kuniona mama yao wakishatuona wanaondoka lakini si kwa kuleta msaada wowote
hivyo naomba wenye uwezo na moyo wanisaidie ili niweze kuwapa malezi
bora’’,alisema Rehema.
Nae Baba wa watoto hao Abubakari Ally
Hamad Mwanajeshi wa ajira mpya katika jeshi la wananchi wa Tanzania [JWTZ]
kikosi cha 673 Msalato Dodoma alisema mahitaji yamekuwa hayatoshelezi kutokana
na mshara anaopata kuishia kwenye madeni ambayo amekuwa akikopa kwa wanajeshi
wenzake.
Alisema pesa hata madeni hayo ambayo
amekuwa akikopa hayatoshelezi mahitaji ya watoto hao ambao hata hivyo hahitaji
kuongeza wengine, hata hivyo aliwataka watu mbalimbali zikiwemo taasisi za
kiserikali kumsaidia kutokana na watakavyojaliwa na mwenyezi mungu ili aweze
kuwa tunza watoto wake.
Kwa upande wake Ofisa mtendaji wa
kijiji cha makulu Namsfu Mihungo alisema wao kama serekali wanajitahidi
kufikisha ujumbe kwa watu kuhusu familia hiyo kuhitaji msaada na kufika kuwaona
lakini hawakujua kama hakuna msaada unaotolewa, hivyo watajipanga kuona nini
watafanya ili kuisadia familia hiyo kwa kadili watakavyoweza.
Rehema Khamis akiwa na watoto wake mapacha watatu na dada
yao ambapo hata hivyo kaka yao hakuwe mwenye umri wa miaka 13, mama huyo
anahitaji msaada ili aweze kuwatunza kuwalea
Rehema Khamis [30] akimlisha uji mtoto mmoja kati ya mapacha
watatu huku wengine wakisubilishwa mpaka wakwanza amalize kutokana na
mama huyo kukosa mtu wa kumsaidi kuwalea watoto hao.
No comments:
Post a Comment