Na John Banda, Dodoma.
SERIKALI imetunga sheria maalumu ya kuwaenzi waasisi wa Taifa ikiwemo kuanza ujenzi wa kituo cha kuwaenzi waasisi hao katika eneo la Kiromo Wilayani bagamoyo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya miaka 14 ya kumbukumbu ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Celina alisema tayari upembuzi yakinifu na athari za kimazingira umeshafanyika katika eneo hilo.
Alisema serikali pia imeshafanikiwa kuzitambua Taasisi, Asasi zinazomiliki kumbukumbu, mali na vitu vyenye umuhimu wa kihistoria kitaifa ili kuvitunzwa vizuri.
Alisema kituo hicho kitakusanya na kuhifadhi kumbukumbu, mali na vitu vyenye umuhimu kihistoria vya waasisi hao kama ilivyoelekezwa katika sheria .
Waziri huyo alisema kituo hicho pia kitaratibu shughuli zote zinazohusu waasisi ikiwemo kuhamasisha umma kuhusu utafiti, kuandaa machapisho mbalimbali yanayoelezea michango na kazi walizowahi kuzifanya waasisi hao.
Aidha alisema serikali imeshaunda Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa kuwaenzi Waasisi wa Taifa ambayo itakuwa na jukumu la kutafuta, kukusanya na kusimamia mfuko huo.
Akizungumza katika Mkutano huo Balozi mstaafu Job Lusinde alisema Mwalimu Nyerere alikuwa ni taasisi pekee kwa mchango wa maisha yake na mafundisho yake ulikuwa mchango mkubwa katika kujenga na kuimarisha umoja na uzalendo.
Lusinde alisema Mwalimu alikuwa mwanasiasa mwenye kipaji cha pekee na aliamiani kuwa siasa kwake ni kuwatumikia watu walikuamini na kukupa dhamana ya kuongoza.
Alisema katika enzi ya uongozi wake Mwalimu Nyerere hakuwa na mchezo na mtu yeyeote katika mambo ya msingi yenye maslahi mapana kwa taifa .
Balozi mstaafu Jobu Lusinde akifafanua jambo mbele ya wananchi
waliokusanyika kushuhudia maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere
kilichotokea mika 14 iliyopita yaliyofanyika katika viwanja vya nyerere Dodoma.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma
Serina Combani akiwa pamoja na viongozi mbalimbali walipokuwa katika
maadhimisho ya miaka 14 ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere yaliyofanyika
katika viwanja vya Nyerere Squere Dodoma jana.
Wanachi waliohudhuria maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha
Mwalimu Julias Kambarage Nyerere wakifuatilia jambo wakati maadhimisho hayo
yakiendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa kwanza wa jimbo la kati Askofu Dr. Saimon
Chiwanga akiwaonyesha wananchi kisiki kilichochipua majani mabichi na
kuwaelezea namna ya kutunza visiki vya miti ya asili bila kuipoteza wakatati
alipokuwa akitoa ushuhuda wa namna alivyomjua Hayati Mwalimu Nyerere katika
maadhimisho yake yaliyofanyika Dodoma.
No comments:
Post a Comment