Monday, September 30, 2013

MAANDAMANO MAKUBWA DODOMA ,WANANCHI WAANDAMANA KUPINGA KITENDO CHA CDA KUBOMOA NYUMBA ZAO.



Na John Banda, Dodoma

WAKAZI wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani mkoani Dodoma wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba.

Wakazi hao walioandamana kutoka Kikuyu hadi Viwanja vya Nyerere Square katikati ya mji wakimtaka mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi kuzungumza nao.

Maandamano hayo yalisindikizwa na ulinzi wa polisi hadi katika viwanja hivyo huku wakazi hao wakiwa wameshikilia mabango yenye jumbe mbalimbali.

Wakazi hao wakiwa wanaimba nyimbo huku wakiinua mabango yao juu yenye ujumbe kama Cda ni zaidi ya Alshababi, CCM mnaiona bomoabomoa, Cda ni zaidi ya Nduli Idd Aminini Dada na lingine likisomeka Hata wanyama hupewa hifadhi.

Wakizunguza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa baadhi ya wananchi na viongozi wao wa mitaa walidai kuwa lengo la maandamano hayo ni kufikisha kilio chao kwa serikali ya mkoa.

Andrew Mdumi mwenyekiti wa mtaa wa Mkalama ambao ni sehemu ya eneo linalotakiwa kuvunjwa alisema kuwa wameamua kufanya maandamano hayo mara baada ya kupewa amri ya kuondoka katika eneo wanaloishi kwa kipindi kirefu.

Mdumi alisema, kuwa Mamlaka ya ustawishi Makao makuu imekuwa ikiwapatia namba kila wakati na kudai kuwa itakuja kuwapimia lakini katika hali ya kushangaza imewapa amri ya kuondoka ndani ya siku saba kwa madai kuwa wamevamia katika eneo hilo ambalo lilikuwewa limetengwa kwajili ya bustani za mbogamboga na matunda.



Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu  [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.




Moja ya bango lenye ujumbe lilotumika katika maandamano hayo


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akipaza sauti ya matumaini kwa wakazi wa Kata ya kikuyu kusini walioandamana kupinga Bomoabomoa ya CDA waliokuwa wamepanga kubomoa nyumba na misingi katika eneo hilo.

WAZIRI WA INDIA ATUPWA JELA KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UMMA.


BIHAR, Jharkhand, India

Mahakama Kuu ya Ranchi nchini India imetoa hukumu 
kwa, Lalu Prasad (66), pamoja na washtakiwa wenzake 44 kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya rushwa wakati alipokuwa waziri mkuu wa Bihar. 

Kesi hiyo iliyovuta hisia za watu wengi Lalu alipatikana na hatia ya matumizi mabaya ya Rupia 37 crore alipokuwa waziri mkuu miaka 17 iliyopita. Hata hivyo hukumu hiyo itatangazwa siku ya Alhamisi kupitia video katika ukumbi wa mahakama hiyo.

Pia alipatikana na kashfa kubwa wakati akiwa kama mtumishi wa serikali kushindwa kuzuia matumizi mabaya ya fedha wakati akiwa waziri mkuu kiasi cha Rupia 950 crores zilizotumika kulipia bili za hewa katika matumizi ya madawa na chakula cha mifugo. Kufuatia hukumu hiyo Lalu amepoteza sifa ya kuwa mwanachama wa bunge, kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama Kuu hivi karibuni.

Washtakiwa wengine ni pamoja na waziri wa zamani 
 Waziri Mkuu wa zamani Mishra Jagannath pia alipatikana na hatia katika mahakama hiyo ya Juu kabisa, pamoja na wanasiasa wengine sita, wawili ambao ni wa chama tawala cha Janata Dal-Muungano. 

Lalu alikuwepo katika mahakama na kuketi wakati hukumu dhidi yake ikisomwa mahakamani hapo, ambapo ametiwa hatia pamoja na watu wengine 44, ikiwa ni pamoja na wanasiasa saba zaidi na watendaji wa serikali wanne

Sunday, September 29, 2013

SAFARI HII JELA YAIKUMBA MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA,YOTE YAFUNGIWA.


SERIKALI imeyafungia  kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba,2013  kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala  za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17 Julai,2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013”  kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri  haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI”  habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa  mkali mwenye hasira.Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.Jambo ambalo halikuwa la  ukweli.

Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.

Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam  mbwa ni najisi hapaswi kuingia  katika maeneo ya ibada.

Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.Gazeti hili limeonywa mara nyingi  lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa  kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za  fani ya Habari.

Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.

Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta  kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika .Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika  na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na  waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.

Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.

Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama  wavione kuwa haviwasaidii.

Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania  kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 septemba,2013,.
Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.

Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.

Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia .Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani  nchini.
Imetolewa na
MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013

Friday, September 27, 2013

WANASIASA ACHENI KAULI ZA UCHOCHEZI ZINAZOASHIRIA UVUNJIFU WA AMANI NCHINI-SOPHIA SIMBA


 Waziri wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akitoa maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya habari hapa nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba wakati akitoa maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya habari hapa nchin