UONGOZI
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wamesema wanakuna vichwa juu ya
jinsi ambavyo watafanikisha kukusanya kodi kutoka kwa wenye nyumba
nchini wanaofanya biashara ya kuzipangisha.
Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitillya alisema jijini hapa mwishoni mwa wiki kwamba kuna changamoto nyingi katika ukusanyaji wa kodi kutoka kwenye nyumba zilizopangishwa.
Alisema ni kawaida kwa kila mtu anayepata fedha kihalali lazima alipe kodi, lakini utaratibu wa kudai kodi kutoka kwenye nyumba zilizopangishwa bado unatafutwa.
“Katika ukusanyaji wa kodi changamoto ipo kwenye kukusanya kodi inayotokana na biashara ya upangisaji, kwa sababu wenye nyumba wengine hawataki kuonyesha mikataba halisi, lakini sasa tumepata wazo tofauti ambalo tunalifanyia kazi ni kutafiti kwamba bei za nyumba za kupanga kulingana na eneo husika, mfano tukijua Masaki wanapangisha nyumba kwa kiasi gani tutakuwa tumepata pa kuanzia, pia tunataka kulifanya suala hili kwa kuhakikisha sheria inatumika ipasavyo,” alisema Kitillya
No comments:
Post a Comment