Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leodeger Chila Tenga,
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wake wa kutangaza
rasmi kutogombea nafasi yake ya Urais wa Shirikisho hilo kwa mara
nyingine, baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka nane, mkutano huo
umefanyika leo katika Ofisi ya TFF, jijini Dar es Salaam leo.
*****************************
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema
hatagombea tena wadhifa huo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika
Februari 24 mwaka huu.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF leo, Rais Tenga amesema
wakati anaingia kwenye uongozi mwaka 2004 ajenda ilikuwa na kuijenga TFF
kama taasisi kwa kuweka mifumo ya uendeshaji ikiwemo kutengeneza katiba
na kanuni, jambo ambalo limefanyika.
“Wajumbe
wamekuwa wakiniuliza Rais vipi? Mimi hapana. Nilishafika pale pa
kufika. Tulipoanza wakati ule ilikuwa ni kujenga taasisi. Na kazi hiyo
tumeifanya. Tulipoingia mwaka 2004 hiyo ndiyo ilikuwa ajenda,” amesema
Rais Tenga.
Amesema
walitengeneza Katiba, vyombo huru vya kufanya uamuzi, kuongeza wigo wa
wapiga kura ambapo hivi sasa kwenye mpira wa miguu hakuwezi kutokea
migogoro, hata ikitokea kuna mfumo wa kuidhibiti.
Rais
Tenga ameishukuru Sekretarieti ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF,
kamati za uchaguzi za wanachama wa TFF na vyama wanachama wa TFF kwa
hatua iliyofikiwa katika uchaguzi ambapo mikoa yote imekamilisha
uchaguzi na kubaki vyama shiriki pekee.
Ametoa
mwito kwa wadau kujitokeza kugombea uongozi TFF, kwani baada ya kujenga
taasisi ajenda iliyobaki ni mpira wa miguu wenyewe ikiwemo nini
kifanyika ili mpira uchezwe katika maeneo mbalimbali.
“Tumeshatengeza
mfumo, sasa ni kuangalia jinsi ya kuendeleza mpira. Changamoto ni
tufanye nini ili mpira uendelee. Tunataka watu wengine wabebe hiyo
ajenda ili tuangalie tunakwendaje mbele,” amesema.
Pia
amesema ushirikiano ambao amepata kwa wapenzi na wadau wa mpira wa
miguu ni wa ajabu. Vilevile ameishukuru vyombo vya habari, Serikali,
klabu, wadhamini na wafadhili kwa mchango wao katika uendeshaji wa mpira
wa miguu nchini.
19 WACHUKUA FOMU UCHAGUZI TFF
Wadau
19 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika
Februari 24 mwaka huu.
Fomu
hizo zimeanza kutolewa leo (Januari 14 mwaka huu) ambapo wawili
wamechukua nafasi ya Makamu wa Rais wakati waliobaki wanaomba ujumbe wa
Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.
Waliochukua
fomu za umakamu wa rais ni Wallace Karia na Ramadhan Nassib. Wote ni
wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF inayomaliza muda wake.
No comments:
Post a Comment