Kikosi
cha Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika
Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili mchana wa
leo kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kwa ajili ya mchezo wao wa
kirafiki wa kimataifa na Yanga ya Dar es Salaam, mchezo utakaochezwa
kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini.
Kikosi
cha Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika
Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waratibu wa mchezo
huos, kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Pichani kushoto ni
Shaffih Dauda, Mmoja wa Wakurugenzi
wa Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga,Mtangazaji wa kipindi cha
Sports Extra,Mbwiga Mbwiguke,Mdau Juma pamoja na Stuart
Nahodha wa timu ya Black
Leopards ya Afrika Kusini akizungumza na wanahabari kutoka vyombo
mbalimbali mara baada ya kuwasili na kikosi chake kizima leo mchana
tayari kwa kupambana na timu ya Yanga Sports Club,kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar.
Waratibu
kutoka Prime Time Promotions Ltd,Shaffih Dauda pamoja na mmoja wa
wakurugenzi wa Kampuni hiyo Godfrey Kusaga wakifanya mawasiliano leo
mchana mara timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini ilipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere..
Shaffih Dauda akiwa ameambatana kocha wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,Abel Makhubele mara baada ya kuwasili leo mchana kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere.
Wachezaji
wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiingia kwenye basi kubwa
la timu ya Yanga,wayatarajia kumenyana nayo hapo kesho kwenye uwanja wa
Taifa,Jijini dar.
Kikosi
cha Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika
Kusini,wakiwasili mapema leo mchana kwa ndege ya shirika la Afrika
Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
====== ======= ======= =======
WAKATI mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga kesho watacheza
mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya Black
Leopards ya Afrika Kusini, kocha wa Black Leopards ametema cheche na
kusema wataibuka na ushindi mkubwa kutokana na uzoefu wao wa mashindano
ya Kimataifa.
Mchezo
huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni na maandalizi yake yamekwisha
kamilika huku waandaaji wakipunguza viingilio ili kuwawezesha mashabiki
wengi kufika.
Mratibu
wa mechi hiyo, Shafii Dauda wa Prime Time promotion alisema jana kuwa
maandalizi yote yamekamilika na wamepunguza kiingilio cha shs 5,000 na
shs 7,000 na kuwa cha shs 3,500 ili kuwafanya mashabiki wengi kuona
mechi hiyo.
Viingilio
vingine ni shs 7,000 kwa viti vya rangi ya machungwa, wakati VIP C ni
shs 15,000 , VIP B shs 20,000 na VIP A shs 30,000
Dauda
alisema kuwa Black Leopards wamewasili na kutamba kushinda mechi hiyo
kutokana na uzoefu waliopata katika mashindano mbali mbali ikiwa pamoja
na kombe la Shirikisho.
Kocha
wa timu hiyo, Abel Makhubela alisema kuwa wanauzoefu wa siku nyingi na
walifanya ziara nchi mbali mbali katika afrika na kuja Tanzania ni moja
ya faraja kwao.
“Ziara
hii ziara yetu ya kwanza Tanzania, tumefanya ziara nchini Zimbabwe na
nchi nyingie, tulipata matokeo mazuri na vile vile tunatarajia kupata
matokeo mazuri hapa, nimekuja na wachezaji wangu wote wa kikosa cha
kwanza, jumla ya wachezaji ni 23, mashabiki watarajie mchezo mzuri,”
alisema Makhubela.
Alisema
kuwa wanaijua Yanga na Simba ni moja ya timu nzuri na maarufu bara la
Afrika na hivyo wamejiandaa kwani ni kipimo kizuri cha ligi ya kwao
ambayo ipo katikati.
No comments:
Post a Comment