Saturday, January 5, 2013

KWA HERI SAJUKI

*RAIS KIKWETE AWAONGOZA WANANCHI KUSHIRIKI MAZISHI YA SAJUKI DAR




Rais Jakaya Kikwete, akiwa makaburini Kisutu leo, wakati akishiriki mazishi ya aliyekuwa msanii wa filam, nchini, Sajuki aliyezikwa leo jijini Dar es Salaam.


Tafakuri makini kabla ya mazishi ya Sajuki leo Januari 4, 2013.
Steve Nyerere mwenye kanzu mbele, Tino (nyuma ya Steve) na waombolezaji wengine wakitafakari kabla mwili kufikishwa kwenye makaburi ya Kisutu na kuzikwa jijini Dar es Salaam leo Januari 4, 2013.


Kwaheri jembe letu Sajuki... msanii Ray akitafakari kabla ya kuzikwa kwa Sajuki leo Januari 4, 2013.
Tangulia mwana... sote tuko nyuma yako Sajuki! Jotti akitafakari kabla ya mazishi ya Sajuki leo Januari 4, 2013.

Single Mtambalike 'Richie' (kushoto) naye aliibuka 'kisheikh' kumsindikiza Sajuki leo Januari 4, 2013.  
Chuzi naye alikuwepo na mtoko wake wa Kisheikh.

Kwaheri mwanangu Sajuki... msanii nyota wa filamu, Mzee Chillo naye alikuwapo kumzika Sajuki leo Januari 4, 2013.

Hivi ni kweli umeondoka Sajuki? Siamini!
Mtangazaji Benny Kinyaiya hakubaki nyuma kumsindikiza Sajuki leo Januari 4, 2013.
Msanii Jimmy Mponda a.k.a Jimmy Master alikuwa akimuaga Sajuki kwa staili yake. 
Mhe. Zitto Kabwe (wa pili kushoto) akitafakari jambo na wasanii na waombolezaji wengine katika makaburi ya Kisutu kabla ya kuzikwa kwa Sajuki leo Januari 4, 2013.
Kwaheri kijana wangu....! Msanii nyota wa filamu, Mzee Magali (kulia) akionekana mwenye majonzi tele kabla ya kuzikwa kwa mwenzao Sajuki leo Januari 4, 2013.  
Said Fella (kushoto) na Chege pia walikuwapon
Ni huzuni kubwa kwa kifo cha mpendwa wetu Sajuki... Mungu amlaze pema! Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Iddi Azzan.
Hapa kabla ya kuwasili kwa mwili kwenye makaburi ya Kisutu leo Januari 4, 2013.







Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa viongozi tele wa serikali na vyama vya siasa waliojitokeza katika mazishi ya msanii nyota wa filamu nchini, Juma Kilowoko 'Sajuki' aliyefariki juzi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi wengine wa kisiasa walioungana na wasanii na Watanzania wengine kibao katika kumsindikiza Sajuki kwenye nyumba yake ya milele leo baada ya swala ya Ijumaa ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mhe. Zitto Kabwe na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Iddi Azzan.
Wasanii wa filamu, muziki na watangazaji wa redio na luninga waliokuwapo ni pamoja na Mzee Magali, Ray, Mzee Chillo, Jotti, Richie, Cheni, Mpoki, Mac Reggan, Chegge, Ben Kinyaiya, Dulla wa East Africa Radio, Said Fella na wengine kibaaaaaaaao....!
Shughuli zote za msiba wa Sajuki zilifanyika nyumbani kwake Tabata Bima kabla baadaye jeneza lake kupelekwa katika makaburi ya Kisutu na kuzikwa mara tu baada ya swala ya Ijumaa.
Marehemu ameacha mke ambaye ni msanii wa filamu pia aitwaye Wastara na mtoto mmoja.
Innalillahi Wa Innaillaihhi Rajjiuuun...(Sisi ni wa Mwenyezimungu, kwake yeye tutarejea na atatupa jaza yake)... Aaaamin!!

No comments:

Post a Comment