Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisoma hotuba yake wakati
alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya
Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo
yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake Mama Asha amewahasa vijana hususan wanafunzi hao
waliohitimu masomo kutokukubali kutumika na watu wenye maslahi binafsi
na kujikuwa wakisababisha uvunjifu wa amani. Aidha amewataka
kutojihusisha na makundi yanayochochea uvunjifu wa amani bila kujitambua
wafanyalo, badala yake amewambo kuwa wakipima kila wanaloambiwa kuwa
linamaslahi na dini yao ama maslahi kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Latifah Nuhu,
wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya
ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo
yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Mwinga Gwao,
wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya
ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo
yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment