Wednesday, January 2, 2013
*WAZIRI FENELLA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA SAJUKI, SHUGHULI ZA MSIBA ZINAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU TABATA BIMA
Ndugu,
jamaa na marafiki wa karibu wa Msanii Sajuki, wakiwa katika maombolezo
ya msiba wa kipenzi chao, nyumbani kwa marehemu Tabata Bima, Dar es
Salaam, leo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangaraamewatumia
salamu za rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo
cha msanii Juma Kilowoko (SAJUKI) kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe
02/01/2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa
iliyotolewa leo, jijini Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na
Utamauni na Michezo imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za
kifo cha msanii huyo na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia
ya filamu hapa nchini.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa
tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.
“Nimepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya
kuelezea masikitiko na huzuni nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika
tasnia ya filamu za michezo ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.
Dkt.
Mukungara amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na
watumilivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa
Mwenyezi Mungu.
Juma
Kilowoko (SAJUKI)ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza
kujihusisha na masuala ya maigizo alipojiunga na kikundi cha Kaole na
baadaye filamu. Filamu alizocheza ni pamoja na Revenge ya Kampuni ya RJ .
Mwaka 2008 aliamua kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza iitwayo Two Brothers kwa kushirikiana na Shija Deogratious ilitoka.
Sajuki baadaye aliamua kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY Production
Company ambapo alitengeneza filamu nyingi zikiwemo Mboni Yangu, Round,
Briefcase , Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077( Zero Seven
Seven).nk
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya
kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki
amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.
Sajuki
alianza kuugua mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo
alikwenda kutibiwa nchini India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu
walifanikiwa kutoa michango mbalimbali iliyomwezesha Sajuki kupata
matibabu yake. Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo
lilileta matumaini na furaha kwa watanzania; aliporejea tu aliweza
kutoa filamu iitwayo Kivuli huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya utengenezaji.
Aidha
hali yake ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili hadi umauti ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe
02/01/2013
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen
********************************
MATUKIO KATIKA PICHA MAPOKEZI YA HABARI YA MSIBA WA SAJUKI,TABATA.
Dada wa marehemu Sajuki akilia kwa uchungu.
Bibi wa marehemu Sajuki akiwasili msibani leo.
Pichani juu ni baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki', Tabata- Bima jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment