Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia Baraza la Sanaa
la Taifa, limebariki kufanyika kwa Fainali za Taifa za Miss Utalii
Tanzania 2012/13 baada ya kuridhishwa na maandalizi yaliyo fanywa na
Miss Tourism Tanzania Organisation waandaaji wenye dhima ya kikomo ya
kuandaa na kuendesha mashindano hayo kitaifa na kimataifa, pia kwa
kuzingatia sheria za nchi, kanuni na Taratibu za mashindano.
Serikali pia imeridhishwa na jinsi Fainali za ngazi za mikoa na kanda
zilivyofanyika kwa mafanikio,ambapo kila mkoa umepata washindi wenye
sifa za kuwakilisha mkoa husika katika Fainali za Taifa mwaka
huu,ambapo jumla ya warembo 60 waingia rasmi kambini kesho katika
hoteli ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam, kuanza mbio za kuwania Taji
hilo la Taifa.
Washindi wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika
mashindano mbalimbali ya Dunia yakiwemo ya International Miss Tourism
World, Miss Tourism United Nation, Miss Heritage World, Miss Tourism
University World, Miss Globe International n.k
Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya
Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss
Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism
Model Of The World 2008-Personality n.k
Fainali za Taifa mwaka huu zimepangwa kufanyika wiki ya kwanza ya
Februari ,wilaya ya Temeke na mkoa wa Dar es Salaam ukiwa umepewa
heshima ya kuwa wenyeji wa Fainali hizo.
Erasto Gideon Chipungahelo
Rai
No comments:
Post a Comment