Thursday, January 31, 2013

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA JANA, PINDA AWATAKA WANAMTWARA KUWA WATULIVU

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia)  akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, ambapo alieleza  taarifa mbalimbali kuhusu ziara yake  Mkoani  Mtwara kuhusu kusikiliza maoni ya wananchi wa Mtwara katika sakata la gesi. Waziri Mkuu amewaomba Viongozi wa Mkoa huo kuwashirikisha wananchi katika mambo mbalimbali. Aidha amewaomba wana Mtwara kuwa watulivu na amewahakikishia usalama na amani itaendeelea kupatikana mkoani hapo (kulia) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi.
 Naibu Waziri wa  Nishati na Madini, George Simbachawene, akijibu hoja mballimbali za Wizara yake leo Bungeni mjini Dodoma.
 Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe (kulia) , Godless Lema (katikati- Aruha mjini) pamoja na Moses Machali (NCCR- Mageuzi- kulia) wakielekean katika ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo. Mbunge  Lema amerudi tena Bungeni  baada ya kushinda kesi yake.
 Baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakielekea ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Wabunge wa Iramba  Magharibi Mwingulu Nchemba(kulia),Joseph Selasini( wa Rombo akiwa katikati), na Mbunge wa NCCR- MAGEUZI, Moses Machali wakiwa katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

No comments:

Post a Comment