“Kuna baadhi ya watu wanatumia vigezo vya kidini kwa ajili ya kufanya vurugu za kuhatarisha amani, Serikali haitaweza kuwavumilia, badala yake tutatumia njia mbalimbali RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa mtindo wa kufanya fujo na kusababisha uvunjifu wa amani kwa visingizio vya dini nchini ni biashara inayolipa na ndiyo maana...
Thursday, January 31, 2013
JK-Tunajua biashara ya dini inalipa, lakini msiivuruge Tanzania
“Kuna baadhi ya watu wanatumia vigezo vya kidini kwa ajili ya kufanya vurugu za kuhatarisha amani, Serikali haitaweza kuwavumilia, badala yake tutatumia njia mbalimbali RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa mtindo wa kufanya fujo na kusababisha uvunjifu wa amani kwa visingizio vya dini nchini ni biashara inayolipa na ndiyo maana...
Makubwa Haya; " Haya, Nani Anauzika Sokoni?!"
Nimeyakuta Kisolanza, Mufindi, hivi karibuni. Ama, tembea ujionee!
MAMBO YA KANGA MOKO HAYOOOOO.
WANANCHI WA WILAYA YA KILWA LINDI, WAANZA KUNUFAIKA NA MRADI WA GESI ASILIA
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega, (kushoto) akishuhudia zoezi la utiaji wa sahihi wa mkataba huo wa miaka mitatu kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Addo Mapunda akitiliana saini na Mratibu wa Mradi wa mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa (Techonoroji Enhanced Edcation) TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo Bi Anne Devilliers, wakati wa hafla hiyo fupi ya kutiliana saini iliyofanyika leo. |
Makabidhiano
RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS KABILA IKULU, AMSINDIKIZA MGENI WAKE LEO
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Joseph Kabila Rais wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kufanya naye mazungumzo
Ikulu jijini Dar es salaam jana jioni.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimsidikiza Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati akiondoka Ikulu Dar es Salaam, jana.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimsidikiza Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es
salaam jioni hii ya Januari 30. 2013. PICHA NA IKULU
ZIARA YA KINANA WILAYANI KAKONKO MKOANI KIGOMA
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa daraja la Umoja
linalounganisha Kata ya Nyabibuye, Kakonko na vijiji jirani vya Burundi.
alipokuwa katika ziara wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Januari 30,
mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na
maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka
huu mjini Kigoma.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua soko la Kata ya Nyabibuye,
Kakonko leo Januari 30, 2013, ikiwa ni ziara ya Katibu Mkuu inayoambana
na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3,
mwaka huu mjini Kigoma. Kushoto ni diwani wa kata hiyo Steven Mnigakiko
na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kakonko Peter Toima.
Wananchi
wa rika zote wa Kijiji cha Rumashi, Kata ya Nyabibuye, wilayani
Kakonko, Kigoma wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahma Kinana
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Januari 30, 2013,katika
kijiji hicho, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na
maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka
huu mjini Kigoma.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Rumashi, Kata ya Nyabibuye, wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, ikiwa ni
sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya
CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma.
Kinana
akiwasalimia wanafunzi wa shule hiyo ya Nyamtukuza wilayani Kakonko
mkoani Kigoma, akiwa katika ziara ambayo ni sehemu ya ziara ya Katibu
Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake
ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo Amani
Ntibakiza.
Kinana
akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo ya Nyamtukuza wilayani Kakonko
mkoani Kigoma, akiwa katika ziara ambayo ni sehemu ya ziara ya Katibu
Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake
ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari
ya Nyamtukuza wilayani Kakonko mkoa wa Kigoma, akiwa katika ziara
ambayo ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya
miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini
Kigoma.
Daraja la Umoja linalojengwa kuunganisha Kata ya Nyabibuye, Kakonko Tanzania na mkoa wa Changuzo Burundi.
KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA JANA, PINDA AWATAKA WANAMTWARA KUWA WATULIVU
Waziri Mkuu Mizengo
Pinda (kulia) akizungumza na waandishi
wa habari mjini Dodoma jana, ambapo alieleza
taarifa mbalimbali kuhusu ziara yake
Mkoani Mtwara kuhusu kusikiliza
maoni ya wananchi wa Mtwara katika sakata la gesi. Waziri Mkuu amewaomba
Viongozi wa Mkoa huo kuwashirikisha wananchi katika mambo mbalimbali. Aidha amewaomba
wana Mtwara kuwa watulivu na amewahakikishia usalama na amani itaendeelea
kupatikana mkoani hapo (kulia) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.
Emmanuel Nchimbi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akijibu hoja mballimbali
za Wizara yake leo Bungeni mjini Dodoma.
Kiongozi wa Kambi ya
Upinzani Bungeni Freeman Mbowe (kulia) , Godless Lema (katikati- Aruha mjini)
pamoja na Moses Machali (NCCR- Mageuzi- kulia) wakielekean katika ndani ya
Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo. Mbunge
Lema amerudi tena Bungeni baada
ya kushinda kesi yake.
Baadhi ya wabunge wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakielekea ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini
Dodoma.
Wabunge wa
Iramba Magharibi Mwingulu
Nchemba(kulia),Joseph Selasini( wa Rombo akiwa katikati), na Mbunge wa NCCR-
MAGEUZI, Moses Machali wakiwa katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma. Picha
na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
Monday, January 28, 2013
mh.lowassa anusurika ajalini
bongo movies walivyoiteka dar live
KINANA NA MSAFARA WAKE WAKAGUA MATENGENEZO YA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake,
ukiingiwa kwenye eneo la Uwanja wa Ndege wa Kigoma uliopo eneo la
Kipampa, kwa ajili ya kushuhudia maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi
mkubwa wa kiwanja hicho unaoendelea ili kukiongezea uwezo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wafanyakazi kwenye uwanja huo alipowasili.
Meneja wa Uwanja huo, Elipind Tesha (kulia) akimweleza Kinana na ujumbe wake hatua ilipofikiwa katika ujenzi huu, ambapo alisema, umefikia asilimia tisini, na kwamba unaweza ingawa unaweza kuanza kutumika rasmi Aprili mwaka huu, lakini matengenezo yote yatakuwa yamekamilika Juni 2013. Wengine kutoka kushgoto ni, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martin Shigela.
Kinana akimsikilliza Mhandisi Mkazi wa Uwanja huo,Cleopa Mpembeni
(wapili kulia) akimpa maelezo ya kiufundi kuhusu ujenzi unavyoendelea.
Meneja wa Uwanja huo, Elipind Tesha (kulia) akimweleza Kinana na ujumbe wake hatua ilipofikiwa katika ujenzi huu, ambapo alisema, umefikia asilimia tisini, na kwamba unaweza ingawa unaweza kuanza kutumika rasmi Aprili mwaka huu, lakini matengenezo yote yatakuwa yamekamilika Juni 2013. Wengine kutoka kushgoto ni, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martin Shigela.
Wenye nyumba za kupangisha kaeni tayari kulipa kodi!
UONGOZI
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wamesema wanakuna vichwa juu ya
jinsi ambavyo watafanikisha kukusanya kodi kutoka kwa wenye nyumba
nchini wanaofanya biashara ya kuzipangisha.
Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitillya alisema jijini hapa mwishoni mwa wiki kwamba kuna changamoto nyingi katika ukusanyaji wa kodi kutoka kwenye nyumba zilizopangishwa.
Alisema ni kawaida kwa kila mtu anayepata fedha kihalali lazima alipe kodi, lakini utaratibu wa kudai kodi kutoka kwenye nyumba zilizopangishwa bado unatafutwa.
“Katika ukusanyaji wa kodi changamoto ipo kwenye kukusanya kodi inayotokana na biashara ya upangisaji, kwa sababu wenye nyumba wengine hawataki kuonyesha mikataba halisi, lakini sasa tumepata wazo tofauti ambalo tunalifanyia kazi ni kutafiti kwamba bei za nyumba za kupanga kulingana na eneo husika, mfano tukijua Masaki wanapangisha nyumba kwa kiasi gani tutakuwa tumepata pa kuanzia, pia tunataka kulifanya suala hili kwa kuhakikisha sheria inatumika ipasavyo,” alisema Kitillya
LULU APEWA DHAMANA, JE KWA SASA KUWA NJE NI SALAMA?
Mahakama Kuu ya Tanzania, imemwachia kwa dhamama msanii Elizabeth Michael 'Lulu', aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kudaiwa kuuwa bila kukusudia, msanii mwenzake Steven Kanumba, mwaka jana.
Lulu
amepewa dhamana hiyo baada ya Makama kupitia vifungu kadhaa na kuona
kesi yake ya kuua bila kukusudia inamruhusu kupewa dhamana.
Msanii
huyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven
Kanumba - The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila
kukusidia, ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa
mtuhumiwa atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha
maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru
Msanii
Lulu wakati akiwa Mahakamani leo asubuhi alipokuwa akisomewa taratibu
za dhamana yake, ambapo kwa upande wa Mawakili wa Serikali walisema kuwa
hawana pingamizi na dhamana hiyo.
Ikumbukwe
kuwa Msanii huyo aliwahi kuomba ruhusa ya kuhudhuria mazishi ya rafikie
kipenzi, Steven Kanumba, kwenye mazishi yake, wakati alipokuwa rumande,
lakini kwa kuhofia usalama wake vyombo husika viligoma na kuelezea kuwa
usalama wake utakuwa hatarini.
Sasa
je kwa kupewa dhamana msanii huyo hivi sasa ataweza kuishi kwa amani
mtaani kama alivyozoea? na je atahakikishiwa usalama wake popote
aendako? na vipi familia yake imejiandaaje kumlinda kwa kipindi hiki
atakapokuwa nje kwa dhamana? hayo ni miongoni mwa maswali yanayotawala
vichwani kwa wanaoliangala jambo hili kwa jicho la tatu.
Inaaminika
wananchi walio wengi, mashabiki wake na wengineo wana hamu sana ya
kumuona akiwa nje na walikuwa wakimuonea huruma sana msanii huyo kwa
kile kilichomkuta, lakini kwa sasa ni jukumu la kila mmoja wetu aliye
karibu na msanii huyu, na hata kila mmoja kwa wakati wake kumlinda
msanii huyu kwa njia yeyote ile ili asijekutimia ile sehemu ya maneno
yake wakati akiwa rumande, kwa kufanya lolote kwa kuogopa maneno ya
wanajamii.
KUMBE DR ULIMBOKA SHABIKI WA YANGAAAAAAAAAAAA
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao la Mbuyu Twite.
Dkt. Steven Ulimboka, akijumuika na mashabiki wenzake wa Yanga jukwaani, wakati wa mchezo huo.
YANGA YAZIDI KUONYESHA VITU VYA UTURUKI, YAICHAPA TZ PRISONS 3-1
Mshambuliaji
wa Yanga, Jerry Tegete, 'Mkali wa Uturuki', akishangilia bao lake la
pili, huku kipa wa Tanzania Prisons, akishangaa akiwa chini baada ya
kushindwa kuokoa mpira huo uliopigwa na mkali huyo wa Uturuki. katika
dakika ya 82. ambapo bao la kwanza pia lilifungwa na mkali huyo na la
pili lilifungwa na Mbuyu Twite. Hadi mwisho wa mchezo huo Yanga
3-Tanzania Prisons 1.
Simon
Msuva, akipiga krosi, wakati wa mchezo huo wa fungua dimba ya Ligi Kuu
ya Tanzania Bara, mzunguko wa pili kwa upande wa timu hizo, uliochezwa
leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Didier Kavimbangu, akijaribu kutupia, wakati wa mchezo huo, ambapo shuti hilo lilipaa juu ya goli.
Sehemu
ya mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao la tatu lililoizamisha
Tanzania Prisons na kuvunja matumaini ya kusawazisha na kuwafanya
wachezaji wa Prisons, kuanguka kila mara ambapo kila aliyekuwa akianguka
alikuwa ameshikwa na msuli.
Friday, January 25, 2013
SIMBA YA OMAN YAIOGOPA BLACK LEOPARD YAINGIZA KIKOSI CHA PILI NA KUPOKEA KIPIGO KIKALI
Baada ya kipigo cha mara mbili mfululizo kutoka kwa timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, timu ya Black Leopards ya nchini Afrika ya Kusini, leo imepunguza machungu yake kwa kuichapa Simba ya jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0, katika mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo imeelezwa kuwa kutokana na hofu Klabu ya Simba iliwachezesha wachezaji wa timu B, jambo ambalo limewakera hadi mashabiki wa Simba waliokuwapo uwanjani hapo leo, ambapo baadhi ya mashabiki waliohudhuria mtanange huo uwanjani hapo walisikika wakilalama kwa kitendo hicho, ambacho kimeelezwa kuwa ni sehemu ya hofu na dharau.
Katika Kikosi cha simba wameonekana wachezaji wanne tu walio katika kikosi cha kwanza cha ligi kuu. huku wachezaji wote waliobaki wakiwa ni wa kikosi cha pili, ambao wengi wao wakiwa ni watoto
Thursday, January 24, 2013
HIII NDIO YANGAAAAAAAAAAA
Golikipa
wa timu ya Black Leopards, Posnett Omony, akisota kuokoa mpira
uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete, kwa
njia ya penati.Timu ya Yanga imeibuka kidedea kwa kuinyuka Black
Leopards mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano wa kimataifa wa kirafiki
uliochezwa leo jioni kwenye Uwaja wa CCM Kirumba. Bao la kwanza la Yanga
lilifungwa na Said Bahanuzi.
Wachezaji wa timu Yanga wakishangilia bao la pili lililofungwa na Jerry Tegete, katika kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende (kulia) akipiga krosi huku Moses Kwena wa Black Leopards, akijaribu kumdhibito wakatia wa mchezo huo uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi
kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na
hatimaye kutinga kimiani na kuandika bao la kwanza.
Subscribe to:
Posts (Atom)