Mbunge
wa viti maalum kutoka mkoa wa Mara, Ester Amos Bulaya amesema
ataendeleza vita dhidi ya mtandao wa wafanyabiashara wa madawa ya
kulevya nchini licha ya kupokea vitisho kuwa anaweza kuuawa.
Mbunge
huyo alitoa hoja bungeni kuitaka serikali kufanya mabadiliko ya sheria
ya dawa za kulevya na kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia
wahalifu wa dawa za kulevya.
alisema baada ya kuwalikisha hoja hiyo alipokea zaidi ya jumbe 2,000.
“Nimepata
maoni mbalimbali ya kwenye mitandao,simu nimetumiwa meseji za
kufurahisha na kunitia moyo. Lakini kuna baadhi ya wachache ambao
wanakuwa na hofu kuniambia ‘watakuua, watakutaka kucha’ something like
that. Lakini nilicho waambia hatuwezi kuacha kusema vitu vya msingi
ambavyo vinagusa taifa letu,vinachafua taifa letu katika anga za
kimataifa.Lakini hatuwezi kuacha kuzungumzia mtandao wa madawa ya
kulevya eti kwasababu wanaoneka ni untouchable ni watu wenye fedha,”
alisema
No comments:
Post a Comment