Friday, November 8, 2013

CHADEMA KUSUSIA UCHAGUZI MKUU 2015.



Na John Banda, Dodoma
CHAMA cha Demokrsia na maendeleo [CHADEMA] kimemwambia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwa hawatashiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika 2015 kama katiba itakayotumika haitakua iliyofanyiwa marekebisho.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa chama hicho John Mnyika kwenye mkutano wa Hadhara wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya wajenzi [CHADEMA SQUERE] vilivyopo mjini Dodoma.
Mkurugenzi huyo alisema Chadema hawatashiriki uchaguzi huo kama serekali itatumia katiba isiyofanyiwa marekebisho na kwamba mchakato wa marekebisho hayo unaendelea sasa hautakuwa na maana yoyote.
Alisema ni matarajio ya wananchi kuona mabadiriko ya katiba waliofanya wao yakafanya kazi ndani ya katiba hiyo hasa katika uchaguzi wa 2015 huku wao chadema wakishiriki huku wakiwa na lengo moja tu la kuiondoa CCM madarakani la chama hicho hakitashiriki uchaguzi.
‘’Rais Kikwete ahakikishe katiba mpya iliyofanyiwa marekebisho ndiyo inayotumika la sivyo Chadema hatutashiriki katika uchaguzi huo na serekali itakuwa moja kwa moja imewafanyia kiini macho wananchi wake juu ya maoni yao waliyoyatoa’’, alisema Mnyika
Aidha Mnjika alilishukuru jeshi la polisi kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sharia kutokana na kutoa kibali cha kufanyika kwa mkutano huo kinyume na tamko la mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi aliyewahi kupiga marufuku mikutano ya siasa isifanyike wakati vikao vya bunge vikiendelea.   



Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiwahutubia wananchi wa manispaa
ya Dodaoma alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho
uliofanyika katika viwanja vya wajenzi mjini humo juzi.



Mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa Chadema John Mnyika
akiwafafanulia jambo wananchi wa mji wa Dodoma waliokusanyika kusikili
mkutano wa hadhala ulioandaliwa na chama hicho juzi


Wananchi wa manispaa ya Dodoma wakifuatilia hotuba za viongozi
mbalimbali wa Chadema waliokuwa wakiwahutubia kwenye mkutano wa
hadhara ulliofanyika juzi

No comments:

Post a Comment