Kikundi
cha ngoma cha Hengo toka wilayani kongwa kikionyesha umahili
wa kuimba na kucheza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya kupinga
vitendo vya ukatili wakijinsia yanayofanyika kuanzia Nov 25 mpaka Des
10 2013 mkoani Dodoma
Na John Banda, Dodoma
ASILIMIA %42 ya kesi zilizoripotiwa polisi kwa kipindi cha
miaka minne ni za vipigo kwa wanawake hali inayodhoofisha afya jamii.
Takwimu hiyo iliyotolewa wakati wa uzinduzi wa maadhimisho
ya kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kati ilitolewa na mkurugenzi wa shirika
lisilo la kiserekali linalopinga ukatili wa kijinsia na watoto [AFNET] Bi Sara
Mwaga.
Mkurugenzi huyo alisema kesi zinazoongoza kupokelewa na
jeshi la polisi mkoani hapa ni za vipigo hasa kwa wanawake vinavyofanywa na
wenzi wao katika ndoa na walio katika mahusiano ya kimapenzi.
‘’Bi Sara alisema kuwa kesi za vipigo zinaongoza kwa
asilimia 42, ikifuatiwa na Ubakaji 32.7%, Shamburio la mwili lenye 16.9%
wakati vitendo vya ulawiti ni 7.4.5. ambapo umepungua toka %15 ya mwaka
2012 hali hii inadhoofisha afya ya jamii’’, alisema
Aidha alisema pamoja na takwimu kuonyesha tatizo la ukatili
wa kijinsia kuwa juu kitakwimu lakini hali halisi ni mbaya zaidi kuliko
invyoonekana kutokana na kesi chache sana zinazoripotiwa kwenye vyombo vya dola
hadi hivi sasa.
Alisema pamoja na hilo ni kesi chache kati hizo
zinazoripotiwa zinazofikia mwisho na wahusika kuchukuliwa hatua zinazosihili,
huku akibainisha kuwa tatizo ni watu kutoelewa haki zao na nini cha kufanya ili
kuzidai.
Uzindizi wa Maadhimisho hayo yanayofanyika kwa siku 16
katika ukanda wa kati unashirikisha mikoa iliyoathirika kwa kiasi kikubwa na
tatizo hilo la unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ya Singida, Tabora na Dodoma
|
No comments:
Post a Comment