Wednesday, November 27, 2013

BEATRICE WILLIAM KUTOKA BSS 2011 MPAKA KUIMBA NYIMBO ZA INJILI SASA KUFANYA BONGE LA TAMASHA KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA SIKU YA CHRISMAS,

Mwimbaji wa nyimbo za injili aliyeamua kuokoka akitokea kwenye mziki
wa kizazi kipya aliibuka mwaka mwaka 2011 tokea Bongo Star Seach [BSS]
Beatrice Williamu atatumbuiza kwanye tamasha hilo litakalofanyika
katika uwanja wa jamuhuri Dodoma
Na Mwandishi wetu ,Dodoma

TUMSIFU Rufutu kutoka nchini Kenya aliyeimba na albam yake iliyobebwa
na wimbo wa Mwambie Farao anatarajia kukonga nyoyo za wanadodoma
katika Tamasha la krismas litakalofanyika Des 25 mwaka huu.
Tamasha hilo litakalofanyika katika uwanja wa jamuhuri mjini Dodoma
linatarajia kuwa kivutio kwa wananchi wa mkoa huo kutokana na
kuwahusisha waimbaji wa nyimbo za injli wenye vipaji vya hali ya
Rufutu alisema amejiandaa vya kutosha ili kukonga nyoyo za wapenzi wa                           
nyimbo za injili kutokana na yeye kuwa na hamu kubwa ya kufanya hivyo
huku akifikisha ujumbe wa uhakika wa neno la Mungu.
Aliwataka wapenzi hao kujiandaa vya kutosha kwani siku hiyo ya
kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo mwokozi wa ulimwengu itakuwa ni
siku pekee kwao kwani atawaongoza kumsifu Mungu kwa vitendo vya
uhalisia kupitia ngoma, filimbi na vinubi.
‘’wapenzi wangu waliopo Dodoma pamoja na mikoa jirani wafike kwa wingi
huku wakitarajia kumuona Nabii Mussa mzee wa mwambie Farao wimbo waje
na Viti, Meza na vitu vingine walivyo navyo ili tuelekee kaanani
pamoja kuteka Baraka’’, alisema
Pamoja na msanii huyo Tokea nchi jirani ya Kenya atakaewaongoza watu
kuelekea kaanani ataambatana na waimbaji wengine wa hapa nchini tokea
jijini Dar es saalam akiwemo Beatrice William aliyeanzia Bongo Star
Sech na kuamua kuokoka na kujikita kwenye nyimbo za injili huku
akitamba na wimbo wa akina Delila wapo.
Waimbaji wengine ni pamoja na Sospeter Jonas Mzungu mzee wa Mshumaa na
Marry Sinkala wote toka jijini watakasindikizwa na waimbaji mbalimbali
wa mkoa huo ambao kwa pamoja watakuwa wakilitawala Jukwaa na
kuwaongoza wapenzi wao kwa kumsifu Mungu ipasavyo.
Kwa upande wa waandaji wa Tamasha hilo litakalofanyika katika uwanja
wa jamuhuri, Liberty Promotion Company kupitia kwa msemaji wake mkuu
John Banda alisema wamejiandaa vizuri kukonga nyoyo za wanadodoma kwa
kuwawekea kiingilio cha 2000 kwa 1000 tu ili watu wengi wapate
kushiriki.
Banda Alisema lengo la tamasha hilo ni pamoja na kuwachangia watoto
yatima, wasiojiweza na katika mazingira magumu kutokana na sehemu ya
mapato yatakayopatikana ili kuwawezesha vijana kuifanya Tanzania Bora.



No comments:

Post a Comment