Na John Banda, Dodoma
WANAFUNZI wawili wa chuo cha biashara CBE
Dodoma wamepoteza maisha papo hapo
kwenye ajali baada ya kugonga tela la mizigo lililokwama barabarani baada ya
kuhalibika.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa
1.00 usiku baada ya kugonga tela la lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi
hao walipokuwa wakitokea kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika
katika kijiji cha ihumwa manispaa ya Dodoma.
Mtandao huu ulishuhudia msongamano
mkubwa wa magari katika barabara hiyo iliyopo pembezoni mwa kambi ya jeshi ya
Ihumwa kwa takribani saa zaidi ya tatu kabla ya polisi wa usalama barabarani
kufika na kuongoza utaratibu wa kuondoka.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma
Suzan Kaganda alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa wanafunzi hao
wakati wakiendesha pikipiki hiyo yenye namba za usajili T 420 CCN
waliokuwa wakukitokea barabara ya morogoro kuingia mjini.
Suzan aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso
na Gerger Lwandala wanafunzi wa CBE na kwamba uzembe wa Dereva wa lori hilo
lenye namba za usajili T 477 ABM na huku Tela lake ni T 838 AAZ aliyeliacha
barabrani zaidi ya wiki bila kuweka alama yoyote huku matengenezo ya barabara
hiyo yakiendelea katik eneo hilo.
Aliongeza kuwa miili ya marehemu hao
iliyokuwa imehalibika vibaya kutokana na kufumuka fuvu la kichwa cha aliyekua
dereva wa pikipiki hiyo na ubongo kusambaa katika eneo hilo imehifadhiwa
katika hospital ya mkoa.
Baadhi ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa
msaada katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha
biashara CBE Dodoma
Baadhi ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma walikufa
kutokana na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na mwendo kasi
huku lori hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama yoyote
barabarani hapo.
Miili ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana kabla ya
kuondolewa katika kijiji cha ihumwa barabara ya morogoro Dodoma kabala
ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya mkoa.
No comments:
Post a Comment