Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameunda kamati ya watu watano kuchunguza
suala la kilichotokea Clouds Media siku ya Alhamisi pamoja na Ijumaa
usiku.
Kamati hiyo imeundwa baada ya Waziri
Nape kufanya ziara Clouds Media leo Jumatatu 20/03/2017 na kuzungumza na
uongozi wa Clouds Media kufuatia tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
kutembelea ofisi hizo siku ya Ijumaa usiku akiwa na askari wenye
silaha.
Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti
Dkt. Hassan Abbas Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO, Bw. Deodatusi
Balile Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Ndg. Jesse Kwayu Mhariri
Mtendaji Gazeti la Nipashe, Ndg. Mengida Johannes kutoka Wapo Redio
pamoja Ndg. Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Baada ya kamati hii kufanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha kutoka pande zote mbili Wizara itasema hatua itakazochukua.
Imetolewa na:
Zawadi Msalla
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
No comments:
Post a Comment