Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira aliyeketi katikati
akishuhudia Makamishna wapya wa Uhamiaji wakila kiapo cha Maadili ya
Viongozi wa Utumishi wa Umma baada ya kuvishwa vyeo vipya katika hafla
iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma, Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Balozi Hassan Simba Yahaya na kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Dr. Anna Peter Makakala wote wakishuhudia tukio hilo.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.
Anna Peter Makakala ,akimvisha cheo kipya Kamishna wa Uhamiaji Utawala
na Fedha, Edward Peter Chogero katika hafla iliyofanyika leo katika
ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Anayeshuhudia ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji Chrispin Ngonyani. Tukio
hili linehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja
Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi
Hassan Simba Yahaya.
Kamishna mpya wa Uhamiaji
Divisheni ya Sheria Hannerole Morgan Manyanga akila kiapo cha Utii mbele
ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala katika hafla
iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba Yahaya.
Kamishna wa Tume ya Maadili ya
Utumishi wa Umma , Jaji Mstaafu Harold Nsekela wa kwanza kushoto
akiwaongoza Makamishna wapya wa Uhamiaji kuapa kiapo cha Maadili ya
Viongozi wa Utumishi wa Umma baada ya Makamishna hao wapya kuvalishwa
vyeo vipya katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa
Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Makamishna wapya wa Uhamiaji
wakisaini Fomu za Maadili ya Viongozi wa Umma baada ya Makamishna hao
kula kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma, katika hafla
iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akitoa maelekezo kwa
Makamishna wapya wa Uhamiaji wakati wa hafla ya kuvikwa Vyeo Vipya
iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment