Rais wa Marekani, Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump alilipa kiasi cha dola milioni 38 kama
tozo ya kodi mwaka 2005, huku ikulu ya Washington ikikiri kuwa nyaraka
zilizovuja ni za kweli na kutoa maelezo ya kina kuhusu kodi aliyolipa
kiongozi huyo.
Nyaraka hizi za siri zinazoonesha kiasi
cha kodi alicholipa Donald Trump, zilichapishwa na kuoneshwa kwenye
vyombp vingi vya habari nchini Marekani.
Rais Trump amekataa kuweka hadharani
nyaraka zake za ulipaji kodi na mapato anayoyapata kutokana na biashara
zake, jambo ambalo limevunja utamaduni wa karibu miaka 40 kwa wanasiasa
kuweka wazi mapato na kodi walizolipa kwa Serikali.
Taarifa hii iliyovuja, ni sehemu tu ya
malipo ya kodi aliyoyafanya kwa mwaka mmoja kutoka kwenye nyaraka za
karibu mwongo mmoja uliopita, huku nyaraka yenyewe ikionesha kukanganya.
Ikulu ya White House, imethibitisha
taarifa zilizochapishwa punde tu baada ya kuwekwa wazi na mwandishi wa
habari za uchunguzi, David Cay Johnston, ikulu hiyo ikisema itatoa
taarifa zaidi.
Nyaraka hii hata hivyo imeonekena
kumuunga mkono Trump, ambaye toka awali amekuwa akisisitiza kuwa amelipa
kodi zake sawa na anavyotakiwa kisheria.
Hata hivyo nyaraka hii ya mwaka 2005
inaonesha tu kiasi anachodai, lakini haikuonesha kabisa vyanzo vya
mapato yake, suala ambalo huenda likajibu masuali kuhusu utata wa
biashara zinazofanywa na Trump.
Nyaraka hiyo inaonesha kuwa Trump na mke
wake Melania, wanalipa kiasi cha dola milioni 5.3 kama wanavyotakiwa na
Serikali kuu, kiasi ambacho ni pungufu ya asilimia nne, amesema
mwandishi aliyevujisha nyaraka hiyo.
Mfumo wa AMT uliotumiwa na Trump
ulianzishwa kwa lengo la kuwadhibiti watu matajiri na wafanyabiashara
wakubwa kutotumia mwanya kukwepa kodi, hivyo hii ni kodi ya ziada
wanayolipa, sheria ambayo hata hivyo Trump anataka ibatilishwe.
Johnstone hata hivyo akihojiwa na kituo cha televisheni cha MSNBC, amesema hafahamu mtu aliyevujisha nyaraka hiyo.RFI
No comments:
Post a Comment