Friday, March 31, 2017

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA RAIS MHE.DKT. MAGUFULI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akipiga ngoma mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpigia makofi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakati nyimbo za mataifa mawili (Tanzania na Ethiopia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye jukwaa kwenda kukagua gwaride la Heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mkutano wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi kwa mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu jijini Dar es Salaam.
Shamra shamra zikiendelea wakati wa kuwasili Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikaribishwa kwa kupewa ua na mtoto Xyleen Mapunda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA SPIKA JOB NDUGAI KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE ELLY MACHA

Wednesday, March 29, 2017

RC MAKONDA AWEKWA KITI MOTO BUNGENI DODOMA.


 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akihojiwa Leo mbele ya kamati ya bunge
Na Ofisi ya bunge, Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda leo amehojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusiana na tuhuma za kuingilia haki, uhuru na madaraka ya Bunge.

Mhe. Makonda aliwasili Bungeni  Dodoma majira ya saa nne asubuhi kuitikia wito wa Kamati hiyo uliotokana na Azimio la Bunge  lililotolewa na Bunge, Februari 8, 2017  katika Kikao cha Nane cha Mkutano wa Sita wa Bunge ambapo amehojiwa na kamati hiyo kwa muda wa masaa matatu kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Katika kikao hicho, Bunge liliazimia kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Makonda na Mkuu wa Mkoa wa Arumeru, Mhe. Alexander Mnyeti kuitwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge baada ya Bunge ili kujibu tuhuma hizo.

Akizungumza mara baada ya Kamati hiyo kumaliza kazi yake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. George Mkuchika alisema Kamati hiyo imekutana leo baada ya kuagizwa na Mheshimiwa Spika wa Bunge kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge.

“Tumefanya kikao hiki cha Kamati baada ya kuagizwa na Mhe. Spika kwa kuwa kwa Mujibu wa Kanuni zetu, Kamati hii inakutana pale tu inapoagizwa na Spika wa Bunge,” alisema.

Alisema Mhe. Spika aliiagiza Kamati hiyo imuite Mhe. Makonda mbele ya Kamati  kufuatia azimio hilo la Bunge lililopitishwa  na Bunge Februari 8, ambapo pamoja na mambo mengine Mkuu huyo wa Mkoa alitakiwa kufika mbele ya Kamati kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

Alisema kwa mujibu wa Azimio hilo, Mhe. Makonda alidaiwa kutoa kauli kupitia Televisheni ya Clouds akidai kwamba wabunge wanasinzia Bungeni jambo lililoonekana kwamba ni kudharau Bunge.

“Napenda kutoa taarifa kwamba Mhe. Makonda leo amekuja mbele ya Kamati na ametupa ushirikiano mzuri, tumepokea maelezo yake na Kamati imemaliza kazi yake,” alisema.

Alisema kama ilivyo utaratibu, Kamati yake itakabidhi taarifa yake kwa Mhe. Spika kwa mujibu wa Kanuni ambapo Spika ndiye atakaeamua namna ya kutoa raarifa kuhusu kazi ya Kamati hiyo.
Mwisho.

CCM YAPITISHA RASMI MAJINA YA WANAOWANIA UBUNGE AFRIKA MASHARIKI.




DA
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM leo jijini Dar es Salaam.
DA 2
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiwa pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho jijini Dar es Salaam.
DA 4
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
DA 5
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM Dkt. Salim Ahmed Salim mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

Tuesday, March 28, 2017

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA PROF PALAMAGAMBA KABUDI AWASILI OFISINI MJINI DODOMA.

ZA
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma.
ZA 1
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
ZA 2
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana naNaibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
ZA 3
Waziri wa Katiba na SheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana na Jaji mfawidhi Kanda ya Dodoma Mhe. Mwanaisha Kwariko alipowasili Wizarani mjini Dodoma
ZA 4

MAKAMISHNA WAPYA WA UHAMIAJI WAAPISHWA LEO MJINI DODOMA.

C
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira  aliyeketi katikati akishuhudia Makamishna wapya wa  Uhamiaji wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma baada ya kuvishwa vyeo vipya katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,  Kulia ni Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi  Hassan Simba Yahaya na  kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala wote wakishuhudia tukio hilo.
C 1
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala ,akimvisha cheo kipya Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha,  Edward Peter Chogero  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Anayeshuhudia ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji Chrispin Ngonyani. Tukio hili linehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira  na Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi  Hassan Simba Yahaya.
C 2
Kamishna mpya wa Uhamiaji Divisheni ya Sheria Hannerole Morgan Manyanga akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.  Anna Peter Makakala katika hafla iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira   na Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba Yahaya.
C 3
Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma , Jaji Mstaafu Harold Nsekela wa kwanza kushoto akiwaongoza  Makamishna wapya wa Uhamiaji kuapa  kiapo cha Maadili ya Viongozi wa  Utumishi wa Umma baada ya Makamishna hao wapya kuvalishwa vyeo vipya katika hafla iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
C 4
Makamishna wapya wa Uhamiaji wakisaini Fomu za Maadili ya Viongozi wa Umma baada ya Makamishna hao kula kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma, katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
C 5
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira  akitoa maelekezo kwa Makamishna wapya wa Uhamiaji wakati wa hafla ya kuvikwa Vyeo Vipya   iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
C 6
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira   akizungumza jambo na Makamishna wapya wa Uhamiaji baada ya kumalizika shughuli ya kuapishwa Makamishna hao  leo katika viwanja vya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma

Monday, March 27, 2017

RIPOTI YA FARU JOHN YAKABIDHIWA KWA WAZIRI MKUU.

*Ni ya uchunguzi uliofanywa na Mkemia Mkuu wa Serikali
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa rasmi ya uchunguzi wa kifo cha Faru John kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele ambaye alikuwa akiongoza tume maalum iliyoundwa na Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amepokea taarifa hiyo, leo (Jumatatu, Machi 27, 2017) kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Prof. Manyele amesema tume yake ilifanya uchunguzi wa kifo cha Faru John kwa kupima vinasaba vya sampuli mbalimbali vikiwemo mzoga, fuvu, mifupa, pembe, damu, ngozi na kinyesi kilichokaushwa ambapo ilibainika kuwa vyote ni vya mnyama mmoja, aina ya faru mweusi ambaye ni dume.

Prof. Manyele amesema matokeo hayo yamethibitisha kuwa faru John alikufa katika hifadhi ya Sasakwa Grumeti kwa kukosa matunzo na uangalizi wa karibu.

“Maabara iliyotumika ni ya Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini chini ya usimamizi wa timu ya wataalamu kutoka Tanzania, wachunguzi wa Serikali, chini ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. 

Sababu za kifo chake zilichangiwa na kukosa matunzo na uangalizi wa karibu, kukosa matibabu alipoumwa, mazoea yanayotokana na kutofuata taratibu zilizowekwa kisheria na mapungufu ya kiuongozu kwa Wizara husika, hifadhi na taasisi zake,” amesema.

Prof. Manyele amesema mapungufu waliyoyabaini kutokana na uchunguzi huo ni kutokuwepo kwa kibali rasmi cha kumhamisha Faru John; kukosekana kwa mkataba wa kupokelewa kwa Faru John hifadhi ya Sasakwa Grumeti na kutofuatiliwa kwa afya na maendeleo ya Faru John baada ya kuhamishwa.

Mengine ni uchukuaji holela wa sampuli za wanyama pori kwa lengo la utafiti na kuzisafirisha nje ya nchi; migongano ya kimaslahi kati ya watumishi waliolenga kusimamia taratibu na wale wenye kusimamia maslahi binafsi na uwepo wa taasisi nyingi zenye mamlaka sawa juu ya masuala ya uhifadhi wa wanyamapori.

“Pamoja na kwamba mawasiliano yanaonyesha zoezi hilo liliridhiwa na Wizara, hapakuwepo na kibali rasmi kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori cha kuruhusu kumhamisha Faru John kutoka NCAA kwenda Grumeti,” amesema Prof. Manyele katika ripoti yake.

Akizungumzia kuhusu uchukuaji holela wa sampuli za wanyama pori kwa lengo la utafiti na kuzisafirisha nje ya nchi, Prof. Manyele amesema kumbukumbu za watafiti na aina ya sampuli wanazochukua haziwekwi vizuri na kwamba tume inashauri TAWIRI na TANAPA wapewe msisitizo juu ya umuhimu wa kuzingatia majukumu yao.

Amesema kuna umuhimu wa kudhibiti watafiti na tafiti ili kulinda taarifa muhimu za vinasaba vya wanyamapori (Genetic information) dhidi ya mataifa mengine. 

“TUME inashauri maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ianzishe kitengo cha Sayansi Jinai na Uchunguzi wa Vinasaba vya Wanyamapori (DNA Forensic Wildlife Laboratory) ili Serikali na vyombo vyake iweze kufanya maamuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata ushahidi wa kimahakama katika kesi za jinai zinazohusu wanyamapori (Expert Witness).

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusomewa ripoti huyo, Waziri Mkuu aliishukuru timu ya uchunguzi iliyokuwa chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kazi iliyoifanya ikiwemo kuainisha udhaifu uliokuwemo ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake.

“Ofisi yangu itaipitia taarifa hii ambayo ni kubwa kiasi na kuifanyia kazi. Matokeo ya kazi hiyo, tutayatoa hivi karibuni ili kuonyesha Serikali imeamua kufanya nini juu ya mapendekezo yaliyotolewa.”

Alimtaka Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Bw. Robert Mande, afuatilie mapendekezo yaliyoainishwa na tume hiyo na wayafanyie kazi mapema iwezekanavyo.

Waziri Mkuu aliiunda tume hiyo Desemba 10, mwaka jana baada ya kupokea pembe mbili za faru John na taarifa yenye nyaraka zilizotumika kumhamisha faru huyo. 

Hatua hiyo ilifuatia agizo alolitoa Desemba 6, 2016, akiwa ziarani mkoani Arusha, ambapo alitoa siku mbili na kuutaka uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru John kutoka kwenye hifadhi hiyo.

Alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za makao makuu ya NCAA zilizoko wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
                                  JUMATATU, MACHI 27, 2017

NEY WA MITEGO HUENDI HILI NI MTEGO NA SERIKALI IMEKUPUUZA.



Ndugu zangu,
Kwenye hili la kuruhusu wimbo wa msanii kuchezwa kwa matani yake, na mengine yaongezwe kwenye tungo, Waziri Mwakyembe amefanya yote sahihi.
- Kwamba amelifanya lililoonekana kubwa na lenye madhara kuwa dogo huku akionyesha wazi kuwa Bwana Mkubwa mwenyewe kaliona hilo na wala hana shida nalo.
Yumkini Harrison Mwakyembe anafungua ukurasa mpya. Kwamba Serikali ina mengine ya kuhangaika nayo, na si kila lisemwalo anayesema atingishwe. Na tusubiri tuone.
Wache Waongee!

Sunday, March 26, 2017

SPIKA NDUGAI AKIWA BANDARINI LEO


Moja kati ya habari ambazo zimekuwa zikijadiliwa kwa hivi karibuni ni pamoja na hii ya bandari ya Dar es Salaam kuhusu kubainika kwa makontena 256 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa njiani kusafirishwa kwenda nje ya nchi, siku chache baada ya Rais Magufuli kufanya ziara ya kushitukiza.

Leo March 26 2017 Spika wa Bunge wa Jahmuri ya Muungano Job Ndugai akiambatana na kamati ya bunge ya nishati na madini wametembelea katika bandari ya Dar es salaam lengo likiwa nikutaka kupata ufafanuzi wa kina kuhusu makontena hayo ili bunge kama chombo cha kushauri serikali kuchukua hatua.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Rais Magufuli alibaini makontena 20 yenye mchanga wa dhahabu alipofanya ziara ya kushitukiza lakini baadae mamlaka ya bandari ilibaini makontena mengine 256 yenye mchanga, kitu ambacho kimemshitua spika na kamati ya bunge ya nishati na madini na kuamua kutembelea bandarini.

Tuesday, March 21, 2017

ANGALIA NDEGE INAYOHUDUMIWA NA WANAWAKE TUPU ILIVYOTUA KUTOKA MALAWI.


Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, limefanikiwa kukamilisha safari ya ndege iliyosimamiwa na wanawake pekee.

Ndege hiyo imetua katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es Salaam.
Marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege hiyo wote walikuwa wanawake, na ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kuandaa safari kama hiyo.

Ndege hiyo ilianza safari yake mjini Blantyre na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar es Salaam.
Shirika hilo la ndege, lilisema lengo la kuandaa safari hiyo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".
Ndege hiyo ilikuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.
Bi Mwenifumbo, 24, ambaye alisomea urubani jijini Addis Ababa, Ethiopia amemwambia Munira Hussein wa BBC kwamba alihamasishwa kuwa rubani na baba yake ambaye pia alikuwa rubani

Monday, March 20, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI NA RAIS WA BENKI YA DUNIA DKT. JIM YONG KIM WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAKUTANO YA BARABARA ZA JUU UBUNGO-UBUNGO INTERCHANGE

BCU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za Juu Ubungo Interchange jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipiga makofi.
BC
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kuzindua mitambo na magari yatakayotumika katika ujenzi wa makutano ya barabara za juu za Ubungo (Ubungo interchange) jijini Dar es Salaam.
BC 1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Crispianus Ako aliyekuwa akielezea nama ya ujenzi huo makutano ya barabara za juu za Ubungo(Ubungo interchange) zitakavyokuwa.
BV
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati wakielekea kuweka jiwe la msingi ujenzi wa makutano ya  barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BVVVVVVV
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakiwapungia wananchi mkono wakati wakielekea kuweka jiwe la msingi ujenzi wa makutano ya  barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BVU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi hawapo pichani kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi  wa ya  barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BNU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akiwa ndani ya basi la Mwendokasi pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (anayetazama kadi yake ya DART) wakati wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BNUUUU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakati wakiwa ndani ya moja ya basi la DART wakati wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BVM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha  Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
BVUUU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza  na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
VUKU
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
NUUU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakati wakiagana na wananchi wa Kivukoni hawapo pichani kabla ya kupanda Basi la Mwendokasi (DART) kuelekea Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi Mradi wa Makutano ya barabara za juu za Ubungo jijini Dar es Salaam.
BVMM
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kutoa hotuba yake kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
VCC

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipanda basi la DART-Maarufu kama Mabasi ya Mwendokasi katika eneo la Kivukoni wakati akielekea Ubungo kuhudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BVN
Picha namba 19. Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa ndani ya basi la Mwendokasi wakati akielekea Ubungo kuhudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam
BCC
 Baadhi ya Wananchi wakifatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuweka jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam-PICHA NA IKULU