Friday, May 31, 2013

WENJE ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI AWAVURUGA CUFNA HOTUBA YAKE.

 Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, leo amechafua hali ya hewa bungeni baada ya kusoma hotuba yaake iliyowakasirisha wapinzani wenzao wa Chama cha CUF, jambo lililomfanya Naibu Spika Job Ndugai, kuahirisha Kikao cha Bunge mapema asubuhi.

Wabunge wa Chama cha CUF wamezua tafrani hiyo Bungeni mjini Dodoma leo wakati Mbunge huyo wa Nyamagana, akisoma hotuba ya Kambi ya Upinzani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wenje akiendelea kusoma hotuba hiyo  ndipo Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdalla Salim, aliomba muongozao kwa Naibu Spika, Job Ndugai,  akipinga maneno yaliyokuwa yameandikwa katika ukurasa wa nane wa hotuba hiyo yaliyosomeka Hivi:- 

Mheshimiwa Spika wa Upande wa CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na kupigania haki za ndoa ya Jinsia moja, usagaji na ushoga hii ni kwa mujibu wa tangazo lao la kwenye mtandao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, ikiungwa mkono na Waziri wa Haki na usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka Chama cha Libera Democratis.

Baada ya hapo wabunge wa Cuf walisimama na kusema wakitaka maneno hayo yafutwe ingawa msomaji wa hotuba hiyo alikuwa hajafika katika ukurasa huo wa hotuba wakati huo msomaji alikuwa amefika kwenye ukurasa wa nne.

Baada ya kuona mabishano na kutoelewana ukumbini humo, Naibu Spika , Job Ndugai, alitumia busara zake na kutangaza kusitisha shughuli za Bunge  kabla mambo hayajawa mabaya maana kulikuwa na kila dalili za kuanza kushikana mashati baada ya baadhi ya wabunge wa Chama hicho kuanza kufoka kwa sauti kubwa ndani ya Bunge, bila kufuata utaratibu

No comments:

Post a Comment