WAZIRI WA AFYA MH DKT. HUSSEIN MWINYI.
SERIKALI imewaagiza watendaji na wananchi kupitia kamati za o za afya kuhakikisha misamaha inatolewa kwa wote wanaostahili.
Aidha imesema kuwa kituo ambacho hakifanyi vizuri katika ukusanyaji na udhibiti wa matumizi ya fedha zinazotokana
kutoa huduma kwa wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF),
viongozi husika wapewe onyo. Baada ya muda watakaopewa iwapo hakuna
mabadiliko zichukuliwe hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuondolewa madaraka waliyopewa.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi wakati akifungua mkutano wa mkutano mkuu wa mwaka wa waganga
wakuu wa mikoa , wilaya na baadhi wa wakurungezi wa hospitali za rufaa
na taasisi za wizara hiyo wakiwemo wakurugnezi wa asasi za kiraia, wadau
wa maendeleo na washiriki kutoka Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI).
Mkutano huo wa siku tatu umefanyik katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper mjini Dodoma.
“Mwongozo wa Serikali kuhusu sera ya ucahangiajia wa huduma za afya nchini unajulikana.
Lakini kuna vituo ambavyo bado vinaendelea kutoza gharama za uchangiaji wa huduma ,kwa makundi ya watu ambayo sera inaelekeza huduma zitolewe bila malipo. Wizara imekuwa ikilamzimika kujibu malalamiko mengi kuhusu vituo ambavyo havitekelezi maelezo hayo,
Nimeambiwa kuwa katika ukusanayaji wa fedha zinazotokana na kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF , vituo binafsi vinaongoza kupata fedha nyingi kuliko umaa pamoja na ukweli kwamba wana wagonjwa wachache wanaohudumia.
Naamini tunajua sababu “alisema Dk. Mwinyi.
Hata hivyo alisema wongozo huo unapitiwa ili uendane na mahitaji ya kisasa.
“Tunajua
umuhimu wa vituo vyetu kuwa fedha za kutosha kwa ajili ya kutoa huduma
bora kwa wananchi hivyo sisi viongozi lazima tutumie njia zote halali za kupata fedha ,pia tuweke usimamizi madhubuti wa kukusanya na kutumia fedha hizo, endapo hakutakuwa na udhibiti imara uboresahji wa huduma hautakuwepo hata kama kuna fedha nyingi,” alissitiza.
Alisema
kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Usimamizi Bora wa Utendajia Kazi ndiyo
nguzo Kuu katika utoaji wa huduma za Afya na Ustawi wa Jamii’. Hivyo
changamoto nyingi zinazojitokeza katika huduma za afya zinaweza kuondolewa na usimamizi na ufuatiliaji wa utendaji kazi wa walio chini.
Dk. Mwinyi aliongeza kuwa tatizo
la upungufu wa watumishi katika vituo vya huduma za afya bado lipo.
Idadi ya watumishi hao waliopo hadio kufikia Aprili mwaka 2013ni 64,449,
ambayo ni asilimia 47 yawanaohitajika katika vituo hivyo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Dk. Rufaro Chatora alisema anampongeza waziri huyo kwa kujibu hojan kwa umahiri na kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo.
Aliongeza
kuwa changamoto za kiafya zinazoikabili nchi ya Tanzania, pia kwa
nyingine duniani. Hivyo rasilimali kila siku hazitoshelezi,
kinachotakiwa ni kuendelea kuboresha huduma hizo.
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo , Regina Kikuli alisema mkutano hu unatoa fursa ya kujadiliana namna ya kuboresha huduma hizo.
Awali
akiwakarisha wageni hao katika mkutano huo,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Rehema Nchimbi alisema mkoa wake umefanikiwa kutekeleza mpango wa
chanjo.
No comments:
Post a Comment