Na
John Banda, Dodoma.
KUFUATIA
kauli iliyotolewa na mbunge wa kilindi Beatrice Shelekindo ya kuwa msikiti wa
barabara ya saba uliopo katika manispaa ya Dodoma unafundisha mafunzo ya ugaidi
na kareti kwa waumini wake imeuathiri msikiti huo.
Akizungumza
na dodomafamily Shekhe Mohamed Awadhi wa msikiti huo alisema kauli yake hiyo
Imeuhathiri waumini wake kutokana kuukimbia na baadhi ya wanafunzi waliokuwa
wakisoma masomo kuhamishwa na wazazi wao.
Awadhi
alisema hivi sasa wapo katika wakati mgumu kutokana na waumini waliokuwa
wakiswali ndani ya msikiti huo kuamua kuhama baada ya kutolewa kauli ambayo
wanaamini ni ya uzushi na uchochezi kwa ajili ya kupotosha jamii na serikali.
Shekhe
huyo alisema kuwa msikiti huo umejengwa kwa miaka mingi na karibu baadhi ya
wanaoswali ni pamoja na viongozi wa kiserikali wakiwemo askari toka taasisi
mbalimbali kama vile polisi,wanajeshi,usalama na takukuru.
“Sasa
kama kweli sisi tungekuwa tunafundisha hayo mafunzo ya ugaidi na
kareti,serikali pamoja na waumini kutoka vyombo vya dola kweli msikiti huo
ungeachwa bila kuchukuliwa hatua zozote”aliuliza Shekhe Awadhi.
Naye
mlezi wa wanafunzi wa msikiti huo wa barabara ya saba Husseni Hamedi
Fundi,alikiri baadhi ya wazazi na walezi kuwahamisha watoto wao kutokana na
kauli iliyotolewa na mbunge huyo wa jimbo la Kilindi.
Fundi
alisema kuwa msikiti unapokea wanafunzi kutoka nje ya Mkoa wa Dodoma kama vile
Kigoma,Singida,Mwanza,Pemba,Zanzibar,Tanga na Bukoba kwa ajili ya
kujifunza lugha ya kiarabu na elimu ya Quran.
“Lakini
hivi sasa baadhi yao wamehamishwa na wazazi, walezi hii yote ni kutokana na
uzushi uliotolewa na Mbunge huyo wa Kilindi ambaye sisi kama waumini wa msikiti
huo tunaona amepotosha jamii na serikali yetu,
''Kutokana
na kauli yake hiyo imetudhalilisha sana hivyo tunaamini Mwanamama huyo
anatakiwa kusema ukweli ukizingatia kuwa sehemu anayoielezea ni Bunge ambalo
linalotengemewa na Watanzania wote'', Alisema Fundi
Kauli hiyo iliyoleta utata ilitolewa
na Mbunge wa jimbo la Kilindi Beatrice Shelukindo mei 4, mwaka huu wakati
akichangia bajeti ya Wizara ya mambo ya ndani alisema msikiti huo wa barabara
ya saba unatoa mafunzo ya ugaidi na kareti.
No comments:
Post a Comment