Pichani
ni moja ya mitaa ya Mtwara iliyoathirka na vurugu za leo, kwa kuchomwa
matairi Barabarani, na kuharibu nyumba za wananchi na Ofisi za Serikali.
*******************************************
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
MTU
mmoja amepoteza maisha, Wanne kujeruhiwa na 21 kutiwa mbaroni kufuatia
vurugu zilizotokea leo Mkoani Mtwara baada ya Wananchi wa Mkoa huo
kufunga baadhi ya mitaa na kuchoma matairi katika Barabara ya Zambia
huku wakiharibu mali za wananchi na kuchoma Ofisi za Serikali pamoja na
Nyumba ya Mwandishi wa Habari wa TBC.
Wananchi
hao walianza kufanya vurugu hizo mara tu baada ya kusomwa kwa Bajeti ya
Wizara ya Nishati na Madini Bungeni mjini Dodoma leo, ambapo walikuwa
wakipinga kile kilichoelezwa kutengwa kwa Bajeti ya Ujenzi wa Bomba la
kusafirishia Gesi kutoka mkoani humo hadi Jijini Dar es Salaam.
Wananchi hao walianza vurugu hizo kwa kuvunja Daraja la Mikindani ambalo ni muhimu kwa mawasiliano kutoka Lindi na Dar kuingia Mtwara.
Aidha
Imeelezwa kuwa katika harakati za kuongeza nguvu ya askari wa kudhibiti
vurugu hizo, gari la Polisi limepinduka wakati likiwa katika mwendo
mkali kuelekea Mtwara na kujeruhi baadhi ya askari.
Baadhi ya Ofisi zilizochomwa moto ni pamoja na Jengo la Ofisi ya CCM saba saba, Hotel
Shengena, ambayo imeelezwa kuwa ni moja ya Hoteli waliyofikia Askari wa
Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwa ajili ya kuongeza
nguvu ya Operation ya vurugu hizo zinazoendelea.
No comments:
Post a Comment