Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo iliyokuwa ikisomwa na Msemaji (Waziri Kivuli wa
Wizara hiyo) ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) Joseph
Mbilinyi ‘Sugu’ Bungeni imesimamishwa kwa kile kilechoelezwa kukiuka
taratibu za Bunge.
Akisimama
kuomba Muongozo wa Spika, Mbunge wa CCM jimbo la Mbozi Mashariki,
Godfrey Weston Zambi, aliliambia Bunge kuwa Hotuba hiyo katika kurasa
zake 12 za awali imejaa maneno ya uchochezi kwa Serikali ya CCM.
Zambi
alisema miongoni mwa maneno hayo ya Uchochezi ni yale ya kusema kuwa
Serikali ya CCM kuwashambulia wanahabari kwa kuwapiga, kuwang’oa kucha,
kuwamwagia tindi kali na kuwaua jambo ambalo sio kweli.
Kufuatia
hatua hiyo Spika wa Bunge Anne Makinda alipokea Mwongozo huo na
kuliahirisha Bunge hadi Hotuba hiyo itakapo pitiwa upya ndipo iletwe
tena Bunge hapo.
No comments:
Post a Comment