Sunday, May 19, 2013

Anglikana Tanzania Lamsimika Askofu Mkuu wa Sita, Dk Erasto Chimeledya

Dk. Jacob Chimeledya akipongezwa baada ya kusimikwa

KANISA la Anglikana Tanzania limemsimika Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa hilo, Dk Jacob Erasto Chimeledya kuwa askofu Mkuu wa Sita wa Anglikana nchini. Ibada ya kumsimika askofu mkuu Chimeledya inafanika muda huu na kuongozwa na aliyekuwa kiongozi mkuu wa kanisa hilo, Askofu Dk. Valentine Mokiwa ambaye amerithiwa na Chimeledya.
Ibada ya kumsimika kiongozi huyo mpya inayofanyika katika Kanisa Kuu Roho Mtakatifu Dodoma inahudhuriwa pia na Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge la Tanzania, maaskofu wa Dayosisi anuai za kanisa la Anglikana Tanzania, pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi.
Askofu Dk. Mokiwa ambaye awali alikuwa akishikilia nafasi hiyo kwa sasa anabaki kuwa askofu wa Dayosisi ya kanisa hilo Dar es Salaam kwa muda wa miaka mitano tena kabla ya mabadiliko ya kufanyika uchaguzi mpya wa nafasi hiyo katika Dayosisi aliyopo kwa sasa.
Miongoni mwa shughuli muhimu ambazo zimeambatana katika ibada hiyo ni askofu mkuu mpya kula kiapo cha kuliongoza kanisa hilo kiimani kwa kujitoa pasipo kwenda kinyume na mwongozo wake, maaskofu wa dayosisi zote kula kiapo cha kumtii na kumpa ushirikiano katika uongozi wake pamoja na waumini kuapa pia, kabla ya askofu Dk. Chimeledya kusaini hati za viapo kuridhia majukumu mapya aliyopewa na Kanisa.
Mtandao huu utaendelea kuwaletea yanayojiri katika ibada hiyo.

No comments:

Post a Comment