Friday, May 31, 2013
CHADEMA NA CUF WAOMBA RADHI KWA VURUGU BUNGENI
Dodoma, Tanzania.Chama cha CUF na Chadema hivi punde Bungeni , vimekubali kuomba radhi kutokana na vurugu zilizosababishwa na CUF yenye mrengo wa Kiliberali na Chadema imemafanya hivyo kutokana na kuihusisha CUF na masuala ya ushoga na usagaji.
Vyama hivyo vimeomba radhi baada ya Kamati ya Maadili ya Bunge kufanya kikao kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 2:30 usiku na kukubaliana kila chama kumuomba spika radhi na pia kuliomba Bunge radhi kutokana na vurugu za jana.
CUF wamelazimika kumuomba spika radhi; kuomba radhi Bunge na kuwaomba radhi Chadema kwa kumtukana Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekeil Wenje wakati akisoma hutuba yake ambayo ndani yake ilieleza sera za mrengo wa Kiliberali ambazo pamoja na mambo mengine ni ushoga na usagaji.
Awali Mnadhimu wa Chama cha CUF, Rashidi wakati akiomba radhi aliipongeza Kamati ya Maadili na Chadema kwa kufikia muafaka kwa maslahi ya Taifa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“ Napenda kuomba radhi kwa watu wote walioumizwa na vurugu za jana,” amesema hivi punde Rashidi.
Naye Kiongozi wa Kambi rasni ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesimama Bungeni hivi pinde na kuwaomba radhi CUF, Bunge na Spika kutokana na hotuba ya jana iliyosomwa bungeni jana na Wenje.
Awali kabla ya kuomba radhi leo, Freeman Mbowe jana kwenye kikao cha Kamati ya Maadili ya Bunge, alisema kwamba CUF wanafuata mrengo wa Kiliberali ambao msingi wa sera zao ni shoga na usagaji na kwamba hawakufanya kosa, pia alisema CUF alimdhalilisha Wenje (Chadema), CUF walichana hotuba yao na kuwaudhi na kuwakera Chadema.
Kutokana na hali hiyo CUF walishauriwa kuomba radhi jambo ambali wamelifanya leo asubuhi.
Wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo John Chiligati ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki amesema jana CUF walikiri kwenye kamati hiyo kwamba wao ni wanachama wa mrengo wa Kiliberali, lakini chama chao hakikubaliani na sera zote kama za ushoga na usagaji kwa kuwa serikali imeshatoa msimamo kwamba haiungi mkono masuala hayo
WAUMINI WAUKIMBIA MSIKITI KISA KAULI YA BEATRICE SHELUKINDO BUNGENI.
Na
John Banda, Dodoma.
KUFUATIA
kauli iliyotolewa na mbunge wa kilindi Beatrice Shelekindo ya kuwa msikiti wa
barabara ya saba uliopo katika manispaa ya Dodoma unafundisha mafunzo ya ugaidi
na kareti kwa waumini wake imeuathiri msikiti huo.
Akizungumza
na dodomafamily Shekhe Mohamed Awadhi wa msikiti huo alisema kauli yake hiyo
Imeuhathiri waumini wake kutokana kuukimbia na baadhi ya wanafunzi waliokuwa
wakisoma masomo kuhamishwa na wazazi wao.
Awadhi
alisema hivi sasa wapo katika wakati mgumu kutokana na waumini waliokuwa
wakiswali ndani ya msikiti huo kuamua kuhama baada ya kutolewa kauli ambayo
wanaamini ni ya uzushi na uchochezi kwa ajili ya kupotosha jamii na serikali.
Shekhe
huyo alisema kuwa msikiti huo umejengwa kwa miaka mingi na karibu baadhi ya
wanaoswali ni pamoja na viongozi wa kiserikali wakiwemo askari toka taasisi
mbalimbali kama vile polisi,wanajeshi,usalama na takukuru.
“Sasa
kama kweli sisi tungekuwa tunafundisha hayo mafunzo ya ugaidi na
kareti,serikali pamoja na waumini kutoka vyombo vya dola kweli msikiti huo
ungeachwa bila kuchukuliwa hatua zozote”aliuliza Shekhe Awadhi.
Naye
mlezi wa wanafunzi wa msikiti huo wa barabara ya saba Husseni Hamedi
Fundi,alikiri baadhi ya wazazi na walezi kuwahamisha watoto wao kutokana na
kauli iliyotolewa na mbunge huyo wa jimbo la Kilindi.
Fundi
alisema kuwa msikiti unapokea wanafunzi kutoka nje ya Mkoa wa Dodoma kama vile
Kigoma,Singida,Mwanza,Pemba,Zanzibar,Tanga na Bukoba kwa ajili ya
kujifunza lugha ya kiarabu na elimu ya Quran.
“Lakini
hivi sasa baadhi yao wamehamishwa na wazazi, walezi hii yote ni kutokana na
uzushi uliotolewa na Mbunge huyo wa Kilindi ambaye sisi kama waumini wa msikiti
huo tunaona amepotosha jamii na serikali yetu,
''Kutokana
na kauli yake hiyo imetudhalilisha sana hivyo tunaamini Mwanamama huyo
anatakiwa kusema ukweli ukizingatia kuwa sehemu anayoielezea ni Bunge ambalo
linalotengemewa na Watanzania wote'', Alisema Fundi
Kauli hiyo iliyoleta utata ilitolewa
na Mbunge wa jimbo la Kilindi Beatrice Shelukindo mei 4, mwaka huu wakati
akichangia bajeti ya Wizara ya mambo ya ndani alisema msikiti huo wa barabara
ya saba unatoa mafunzo ya ugaidi na kareti.
WENJE ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI AWAVURUGA CUFNA HOTUBA YAKE.
Mbunge
wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, leo amechafua hali ya hewa bungeni baada
ya kusoma hotuba yaake iliyowakasirisha wapinzani wenzao wa Chama cha
CUF, jambo lililomfanya Naibu Spika Job Ndugai, kuahirisha Kikao cha
Bunge mapema asubuhi.
Wabunge
wa Chama cha CUF wamezua tafrani hiyo Bungeni mjini Dodoma leo wakati
Mbunge huyo wa Nyamagana, akisoma hotuba ya Kambi ya Upinzani ya Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wenje
akiendelea kusoma hotuba hiyo ndipo Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud
Abdalla Salim, aliomba muongozao kwa Naibu Spika, Job Ndugai, akipinga
maneno yaliyokuwa yameandikwa katika ukurasa wa nane wa hotuba hiyo
yaliyosomeka Hivi:-
Mheshimiwa
Spika wa Upande wa CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa
kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na kupigania
haki za ndoa ya Jinsia moja, usagaji na ushoga hii ni kwa mujibu wa
tangazo lao la kwenye mtandao wa umoja wa maliberali ulimwenguni,
ikiungwa mkono na Waziri wa Haki na usawa wa Uingereza, Lynn
Featherstone kutoka Chama cha Libera Democratis.
Baada
ya hapo wabunge wa Cuf walisimama na kusema wakitaka maneno hayo
yafutwe ingawa msomaji wa hotuba hiyo alikuwa hajafika katika ukurasa
huo wa hotuba wakati huo msomaji alikuwa amefika kwenye ukurasa wa nne.
WAZIRI MKUU AFUNGA SEMINA YA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KUHUSU UTARATIBU WA KUPATA MBOLEA YA RUZUKU KWA WAKULIMA.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimfafanulia jambo Mkuu wa
Wilaya ya Bunda Angelina Mabula nje ya ukumbi wa Royal Village Dodoma walipoku
wakitoka Kwenye Semina ya wakuu wa mikoa, Wilaya na Wabunge kuhusu Mfumo mpya
wa utoaji wa Ruzuku ya Mbolea ya mazao kwa wakulima, iliyoandaliwa na Wizara ya
kilimo na Chakula.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akitoka kufunga Semina ya siku
Mbili iliyofanyika Dodoma jana iliyowahusisha Wabunge, Wakuu wa Mkoa na Wilaya
wa Nchi Nzima Kuhusu Utaratibu mpya wa Utoaji wa Ruzuku ya mbolea ya mazao kwa
Wakulima katikati ni Waziri wa Kilimo na Chakula Christopher Chiza Naibu Waziri
wa wizara hiyo Adamu Malima na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Angelina Mabula
Washiriki wa Semina ya Utaratibu
Mpya wa utoaji wa Ruzuku ya Mbolea Kwa wakulima iliyofanyika mjini Dodoma kwa
siku mbili
PICHA NA
JOHN BANDA
Subscribe to:
Posts (Atom)