Monday, July 14, 2014

SHAKIRA ALIVYONOGESHA USHINDI WA GERMAN KUTWAA KOMBE LA DUNIA DHIDI YA ARGENTINA.






Mshambuliaji wa German Mario Goetze (kushoto) akishangilia bao pekee aliloifungia timu yake dhidi ya Argentina, katika dakika za nyongeza fainali za Kombe la Dunia jana usiku. German ilishinda bao 1-0

TIMU ya Germany, jana usiku imeibuka mabingwa wapya wa michuano ya Kombe la Dunia 2014 'FIFA World Cup', baada ya kuifunga Argentina kwa bao 1-0, katika mchezo wa Fainali za Kombe la Dunia uliochezwa kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro.

Timu hizo zilimaliza dakika 90 bila ya kufungana na kuongezwa dakika 30 ambapo German iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1 lililofungwa na MARIO GOETZE, katika dakika ya 22 kati ya dakika 30 za nyongeza bao lililodumu hadi kumalizika kwa dakika hizo za nyongeza.

Germana wameweza kutwaa Kombe hilo kwa mara ya nne sasa tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo ambapo kwa mara ya kwanza ililinyakuwa mnamo mwaka 1954, 1974, 1990 na hatimaye 2014.
Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Hispania, Carles Puyol, akipozi mbele ya Kombe la Dunia na Mwanamitindo wa Brazil, Gisela Bundchen baada ya kombe hilo kuwasili uwanjani hapo jana kabla ya kuanza kwa fainali hizo

No comments:

Post a Comment